Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna habari zisizothibitishwa kwamba yule Mkurgugenzi aliyehusika katika tukio la mauaji pale kanisani ni Itigi ni mtoto wa dada yake Raisi Magufuli. Ikiwa hili ni kweli basi ni wazi kwamba tukio hili litavuta hisia za wadau wengi kwa sababu mbalimbali na wengi watapenda kuona mwisho wake unakuwaje.
Katika JF kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kwa Mkurugenzi huyu kutumia madaraka yake kimabavu mara kwa mara bila ya kuonekana kuchukuliwa hatua yeyote, au "kutumbuliwa' kama walivyopendekeza wachangiaji mbali mbali katika mitandao ya jamii.
Wakati fulani hata ilionekana Mkurugenzi huyu kumkosoa kwa namna ya kumkaripia Waziri wa Tamiseni Jafo bila woga, akimshutumu kuwa alikuwa anapotosha umma. kitu ambacho kilisemekana ni hali ya kujiamini sana. Katika protokali, si jambo la kawaida kwa mkurugenzi wa ngazi ya halmashauri ya wilaya kumshutumu waziri wake hadharani kama alivyofanya, isipokuwa kama anajua kuna namna fulani analindwa.
Baadhi ya post zilizomhusu huyu Mkurugenzi zilizowekwa humu JF ni kama zifuatazo;
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi amshukia vikali Waziri Jafo kwa kuupotosha umma!
Hivi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwa mauza uza yake yote hajatumbuliwa tu?
Mkurugenzi Halmashauri ya Itigi atishia kuwasweka rumande walimu waliohamishwa kisa madai ya stahiki zao
Eti Meneja wa City Style Hotel naye kawa DED wa Itigi, jamani tuweni serious kama nchi