Pole mkuu
ipo hivi!
Hiv test inapima vinasaba vya hiv kwenye damu. Hivi vinasaba vikiwemo kwenye damu, haviondoki. Hivyo ikiwa aliyepima na akakutwa na vinasaba, hata atumie ARV, vinasaba vitasoma bila kelele.
Sa itakuwaje kutumia ARV?
Anayetumia ARV anapata matokeo makubwa mawili.
1. Anapunguza ujazo wa VVU (viral load) kwenye damu.
2. Anaimarisha umadhubuti wa kinga-mwili dhidi ya VVU (CD4 cells count) zinaongezeka mwilini.
Hii inamaanisha nini?
Kufubaza ongezeko la VVU mwilini pamoja na kuimarisha CD4 cells kunamuepusha mgonjwa dhidi ya magonjwa nyemelezi. Hii inaimarisha quality of life kwa mtu anayeishi na VVU.
Maana ya masomo haya ni nini?
1. Once HIV Positive, ALWAYS HiV positive. Usidanganyike!
2. Utaratibu wa kupima kabla ya kufurahia faragha ya kuingiliana, ndio ujanja huo. Endelea nao.