MWANAHARAKATI MWEMA
JF-Expert Member
- Dec 16, 2022
- 216
- 313
- Thread starter
- #41
Sa
Sasa Kwa staili hiyo huoni kwamba mtu anaweza kupata mchumba wakaenda hospital kupima na kutokana na huyu anayetumia dawa Kwa usahihi kipimo kushindwa kusema atakuwa amejiingiza kwenye hatari ya kuambukizwa Kwa kuwa atamla Kwa kuwa wamepewa majibu ya unditectable.Ndio ni kweli, mtu anayetumia ARV kwa usahihi kwa muda mrefu, hivi vipimo vya rapid test ambavyo ndivyo vinavyouzwa pharmacy na vinapatikana maabara vinaweza vikashindwa ku detect na hatimaye kutoa majibu ya FALSE NEGATIVE.
Kumbuka ARV husababisha wingi wa ujazo wa virusi katika damu kuwa chini sana hatimaye kutokuonekana
UNDETECTABLE.
Pia ikumbukwe kwamba hata mtu aliyepata maambukizi akiwa kwenye window period/ kipindi cha mpito vipimo vya haraka/ rapid test havionyeshi ndio maana unashauriwa kurudia baada ya miezi mitatu hadi Sita.
Hitimisho, maabara za benki za damu au hospitali kubwa wanazo ongezea watu damu wana vipimo ambavyo ni advance zaidi ambavyo vinaweza ku detect maambukizi ya virusi kwa usahihi zaidi tofauti na hivi vya rapid test vinavyotumika tulivyovizoea.