Sio kweli, Once umekua Sero Positive utabakia hivohivo Maisha yako yote.
Namaanisha hivi, vipimo vya HIV vipo vya aina kubwa mbili,
Moja.. Vinavyoangalia Muitikio wa Kinga ya mwili ( Antibodies test ).
Mbili ...Vinavyoangalia Kirusi husika .
Hivi vipimo vyetu Mara nyingi tunatumia aina ya kwanza ( Antibodies Test )....
Iko hivi mtu akipata maambukizi ya HIV, Kinga ya mwili huamza askari wa zana maalum na HIV.... askari Hawa huitwa ANTIBODIES..
Sasa Hawa Askari wakifanya Kwa ajili ya VVU, Huwa hawapotei Tena ,watabakia hapo siku zote za Maisha ya mtu Hata kama anatumia ARV Kwa muda wote na Kwa usahihi.yeye ukimpima kipimo Cha kwanza, ataonekana tu ni mwenye makosa. .
Ila mtu wa aina hii, kwakua anatumia ARV vizuri, huweza Kupunguza kiwango cha kuzaliana Cha VVU kiasi Cha kufikiria hatua inayoitwa "UNDETECTABLE" .. yaan VVU kutokua detected Kwa kutumia Kipimo namba mbili...katika hatua hii Mgonjwa huyu tunamuita STABLE PATIENT.. .yeye ikiwa sababu nyingine chochezi zitabakia kuepukika, basi Uwezo wake wa kuingilia Huwa ni Mdogo .