Ni kweli kwamba private wa jeshi la Marekani ni bora kuliko Generali wa jeshi la Tanzania?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Wakuu, Kuna mjadala ulikua unaendelea mahali huku mtaani, tulikua tunajadili kuhusu ubora wa majeshi ulimwenguni. Jamaa mmoja ambae ni mstaafu wa jwtz akasema kwamba kwa experience yake ya kukaa jeshini karibu miaka 30,anaona private wa jeshi la marekani ni bora kuliko Generali wa jwtz, sababu alizozitoa ni kwamba private wa USA army yeye kwa mwaka anaweza akawa deployed kwenye war zone hata mara tatu, but huku Tanzania Mtu anafikia level ya ujenerali akiwa hata hajawahi kukanyaga war zone yoyote wala kupiganisha vita yoyote.
Je Kuna ukweli hapo wakuu?
 
Vita ni sehemu tu ya majukumu ya kijeshi, si kwamba vita ndiyo kila kitu jeshini. Ni kupitia majukumu hayo wanajeshi hutambuliwa kwa ukakamavu wao. Kusimamia ujenzi wa ukuta wa Mirerani ndani ya muda na gharama ile siyo jambo dogo ni mission kubwa sana ile.

Kingine uelewe kuwa si kila mwanajeshi ukadhani kuwa awapo vitani huwa anajukumu la kurusha risasi, si wote warushao risasi, wengine kazi yao ni kutafuta na kuokoa majeruhi wao tu, wengine kazi yao ni kuwezesha mawasiliano, wengine kazi yao ni kusambaza supplies tu, kuna wengine wapo kwa ajili ya ujenzi tu.
 
Hayo ni matusi makubwa sana. Huyo Askari alikuwa ni nanga kwa miaka yote 30 aliyo kaa jeshini. Hajui hata majukumu ya Private jeshini na afisa mwandamizi kama General. General haendi front line, anaweza kaa mtaa wa Mirambo Upanga akapiganisha vita Butembo au Bunya DR Congo. Vile vile ajue course za msingi wanazo attend Majenerali ni sawa.
 
Generali aliyewahi kupigana vita akiwa Private,Na Generali ambaye toka akiwa Private hajawahi kushiriki vita yoyote hadi anakuwa Generali.Huwezi niambia hawa watu watakuwa sawa katika majukumu yao ya kivita....
 

Na wengine ni madaktari na wauguzi kwa ajili ya kutibu majeruhi
 
hivi Tanzania kuna jeshi au kichekesho?
maluten wao kazi yao ni kushinda chini miembe wanapiga story za madem na pombe tu.bora hata police wa Tanzania kazi yao inaonekana
Tatizo JWTZ halizalishi ndio maana wanayafanya hayo,wabadilike wawe wanafanya pia na uzalishaji,maana kazi wanazofanya sio za jeshi kabisa,ma"KURUTI" ndio wanateseka sana kutwa kufyeka mapori tu.
 
Ninaweza kusema ni kweli kwa baadhi ya mambo ila si kweli moja kwa moja.
Vyeo vya kijeshi dunia mzima vinakwenda sambamba. Na mtu mpaka anakuwa General huyo amepita kwenye vyuo vingi vya ndani na nje. That's why Colonel wa Tz akienda US. hupewa heshima sawia na colonel wa US.
Utofauti wa mjeshi wa Tz na US. uko katika gharama za mafunzo yao tu. Huku bongo ni ma private wangapi wanaweza kurusha jeti za kivita?
Huku bongo ni private wangapi wanajua IT?.
 
Tatizo JWTZ halizalishi ndio maana wanayafanya hayo,wabadilike wawe wanafanya pia na uzalishaji,maana kazi wanazofanya sio za jeshi kabisa,ma"KURUTI" ndio wanateseka sana kutwa kufyeka mapori tu.
mkuu..nilishangaa siku nimeenda pale lugalo naona lutens wamekaa chini ya miti wanapiga soga za madem.nkajiuliza hawa kweli nao ni wanajeshi!
 
Kwenye vyeo vya kijeshi ni sawa wanapeana heshima. Wenzetu wametuzidi kwenye mambo ya IT.Huku Bongo hakuna private anayerusha Jetfighter anayerusha hizo ndege vita, Bongo kuanzia cheo cha Afisa yani kuanzia nyota mbili(Luteni)
 
Marekani ipo field mda wote, wenzako kila sku wapo practical, wanafanya mistake wanajifunza magumu wanayopitia namna ya kuyakabili siku nyingine, hakuna nchi yenye jeshi imara kama marekani mpak sasa tusidanganyane hata kidog.....wengine ni wakimbiza upepo tuu....Ni kichekesho kulinganisha mjeda wa Tz mwenye kitambi na copro wa US, nchi ya kwanza kiuchumi vs nchi ya mwisho kiuchumi how comes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…