Sio nakupiga kamba, nenda popote katika hii nchi kaulize madaktari watakwambia hichi kitu.
Mhitimu (fresh from university) wa udaktari wa binadamu (Md) aliyehitimu USSR ya zamani, Russia ya sasa, Ukraine, China au India hana uwezo kamili wa kutibu mgonjwa kumkaribia mhitimu wa hapa Tanzania hususani kutoka Muhimbili. Na siri ni moja tu, daktari mwanafunzi, tena mgeni kutoka afrika, halafu mwenye ngozi nyeusi hawezi kupewa nafasi kamili ya kujifunza kwa kutibu (clinical practice) kwenye mwili wa mzungu (mrusi), mchina au mhindi.