Ni kweli kwamba Profesa Janabi hajawahi kusomea wala kuwa Daktari Bingwa wa Moyo?

Tatizo mmekariri Hilo dude la mwisho PhD Bioregulatory medical science ndio kila kitu ni zaidi ya hizo Mmed au wenyewe mnaita specialist ..
 
Mwalimu wa biology hapa Tanzania mwenye degree anaweza kusoma masters of science in urology kwa mujibu wa comment uliyoandika?
Hebu Usinifanye Nicheke ndugu yangu Ndo maana Nimeanza na Afya..Mkuu Kwenye Hiyo comment..

Ila Ukizungumzia Urology kwa Tz Ni Super Hiyo Haingiwi Kichwa kichwa Mpaka Uwe Umesoma MMED ya Internal au Paed..

Usione ina Msc basi ukajua Ni Kwenye zile nilizozungumzia MSc na MMED..
Msc ya Urology ni Ubingwa Bobezi
 
🀣🀣 Duuh!

Hebu ngoja wataalamu watujuze. Mwenyewe napata utata hapa.

Maana hapa Bongo elimu za mchongo ni nyingi sana.

Unayemuona ni mtaalamu kumbe na yeye ni wa mchongo.
 
Hili ni kweli kabisa,nimeshuhudia haya.
 
Nakusahihisha.
Professor Janabi alifanya Msc in Tropical health (ambayo mhitimu yoyote wa kada ya afya anaweza kufanya, sio lazima awe Md) na hakufanya Mmed of Tropical medicine.
Msc of tropical health sio sawa na Mmed.
Mimi kilaza wa mambo ya afya naomba nikuelewe hivi mkuu:

1. Msc ya Tropical Medicine sio kigezo sahihi kinachohitajika kwa daktari kwenda ngazi ya kuja kubobea magonjwa ya moyo. Msc hiyo ni hafifu, hata Degree holder wa Pharamacology anaweza soma.

2. Ili mtu akasomee kuwa Cardiologist inabidi kwanza asome Mmed, na sio Msc.

Lakini kwa maelezo ya DR Mambo Jambo ambayo nilichanganya nikadhani Prof. Janabi ana Mmed ya Tropical Medicine kumbe ana Msc ya Tropical Health, je mtu mwenye Msc hiyo (badala ya Mmed) naye ana sifa za kubobea kwenye cardiology?

Wakuu kumbuka mwanzoni hoja ya ndugu Zanzibar-ASP ilikuwa Prof. Janabi hana Mmed ya Internal Medicine hivyo hana sifa. Kwahiyo nikataka kumtetea kuwa hana Mmed ya Internal Medicine ila ana ya Mmed ya Tropical Disease, sasa nazidi kuambiwa pia hana hiyo Mmed bali ana Msc ya Tropical Health.

Nimerudi kwenye CV yake naona MD, Msc. PhD.
Kwahiyo ndugu DR Mambo Jambo nakuuliza tena, Msc ya Tropical Health ya Prof. Janabi inafaa kuwa mbadala wa Mmed ya Tropical Medicine. Ili Zanzibar-ASP aridhike?

Update: Nimekuja kujua hapa kupitia kwa DR Mambo Jambo kuwa Mmed ile ni (Internal medicine Specified In Tropical Medicine). Mwanzoni nilijua Internal Medicine na Tropical Medicine ni vitu viwili tofauti, mnaandika kwa kifupi sana nyie waganga.
 
Asante mkuu.
Mchangiaji hapa anadai Prof. ana Mmed ya Internal Medicine Specified in Tropical Medicine.

Mleta mada ndugu Zanzibar-ASP umedai Prof. Janabi hana Mmed bali ana Msc ya Tropical Health. Mleta mada unaamini uko sahihi na data zako?
 
kumbe mwamba hakuwahi kusomea udaktari bingwa wowote (Mmed) achilia mbali udaktari bingwa wa moyo (Cardiologist) na wala hana sifa zozote stahiki za kibingwa kutibu moyo.
Hivi wewe kwa akili yako, kuna chuo kikuu hapa kwetu ambacho kinaweza kumpa mtu cheo cha mhadhiri (lecturer) na mtu huyo akapanda vyeo hadi kuwa profesa, bila kuwa na elimu ya MMed or equivalent? Yaani unaamini chuo kikuu chetu cha udaktari (MUHAS) kilifanya hivyo kwa Dr Janabi? Kama ni hivyo basi kinapaswa kufutwa kwenye orodha ya vyuo vikuu nchini na duniani.

Tatizo lako ni kwamba hujui kuwa MMed ni equivalent to PhD degree. Terminology ya MMed ni ya hapa kwetu tu, kwingineko duniani hakuna neno kama hilo, kuna PhD tu.
 
Nimetoka kuongea na mchepuko wa mdogo wangu mmoja hupo huko Utete,Rufiji, anaitwa dokta wakati yeye ni mgawa "mbaazi".

Ameongelea hili swala la watu kuwaita madokta wafanyakazi wote wa hospotali/zahanati.
 
Inategemea unafundisha nini, kuna wengine si MD lakini wanafundisha MD hapo MUHAS.
 
Kwani Muhimbili wanafundisha Medicine tuu hakuna programme zingine anazoweza kufundisha?

Na je kwani hata hao wa Medicine si kuna masomo ya biomedical science anaweza kufundisha. Kuwa
lecturer Muhimbili haimpi uhalali wa kuwa na MMED Internal Medicine.
 

Hiyo picha ni kabla gajaanza kunywa supu ya mchicha kama breakfast...?
 

Mabeberu gani wanatoa kazi ya maana kwa mtu asiyekuwa na elimu?

Hospital gani imeajiri daktari asiye na elimu eti kisa ana uwezo?

Uwezo na elimu vinaenda sambamba acheni kujifariji. Unataka WHO iendeshwe na mtu asiye na elimu eti kisa ana uwezo haiwezekani.

Wewe unaweza kubali ufanyiwe operation ya kichwa au yeyote ile na mtu asiye na elimu hiyo kisa tu umeambiwa ana uwezo?

Mambo ya uwezo yaishie kwa fundi juma na fundi maiko wanaoangusha majengo. Mambo ya msingi yaendeshwe na watu wenye elimu ya kutosha na ujuzi.

Ungejua medical field ilivyo over-regulated usingeongea huu utopolo. Naamini Janabi ana vigezo vyote nontheless.
 
Kamanda mbona umeandika kinyume, hiyo nafasi inahitaji mtu mwenye elimu, wewe unasema tuachane na mambo ya kuangalia elimu. Utakua director wa WHO bila kuwa na elimu(mtaalamu wa hilo eneo)?

Hiyo sio nafasi ya mkuu wa mkoa au wilaya. Hiyo ni nafasi ya wenye elimu
 
Tatizo Kubwa Linakuja kuwa Muundo wa Afya Tanzania Hautambui Mchanganyiko ama Course inayoitwa MMED (Internal Medicine Specified In Tropical disease) ila wanaitambua tu ni Kama MSc In Tropical D'se..
Kitu ambacho kwa Tanzania Kinampa Ubingwa Kwenye Tropical Disease Peke yake na wala Hakumpi Ubingwa kwenye Magonjwa yote ya Ndani..

Kwa Tanzania (Muundo ma kanuni za MCT) Atakosa Sifa ya Moja kwa Moja Kusoma Fellowship ya Cardiology ila kwa Nje Anayosifa Hiyo kwa kuwa wanatambua Course hiyo..

Shida Kubwa ni Muundo Maana Tanzania Hawaitambui kama MMED inakosa Sifa Kuwa MMed ila Wanaitambua kama MSc..
 
Muulizieni mpendwa mstaafu wetu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…