Hapa tunazungumzia sifa za kuwa daktari bingwa mbobezi kwa kanuni, taratibu na sheria za baraza la madaktari la Tanganyika (MCT), standard za MCT zinashahabiana mnoo na nchi nyingi za Africa zilizopiga hatua kwenye fani ya utabibu kama Kenya, Ghana, Nigeria, South Africa. Huna Mmed ya internal medicine huna sifa za kusomea ubobezi wa moyo. Na kwa ubingwa ubobezi wa watoto, huna Mmed ya watoto (paediatric) huna ubobezi wa moyo.
Kwa nchi zilizoendelea sana kama USA, UK, Germany, France, Canada mziki wa kuwa Daktari bingwa wa moyo ni mchakato mrefu, mpana na mzito. Kwa alichosomea Professor Janabi huko anaweza kuishia masijala tu akihifadhi kumbukumbu za taarifa ya wagonjwa.