Tetesi: Ni kweli makao Makuu ya Jeshi Dodoma yanajengwa na China?

Tetesi: Ni kweli makao Makuu ya Jeshi Dodoma yanajengwa na China?

Sijajua mantiki ya thread hii ulitakaje kwanza? Uwanja wa ndege wa jeshi kule ngere ngere kule morogoro umejengwa na China kipindi cha Jk
Naelewa hayo ya ngerengere, hoja yangu ni kuwa kwanini vitu kama hivi tusijenge wenyewe? We unafahamu vizuri jeshi lilivyo mahiri katika sekta ya ujenzi. Na hii haijaanza leo nakumbuka miaka ya 80 kulikuwa na daraja la mkoloni pale old bagamoyo road lililotaka kuvunjika. Jeshi wakalijenga la muda chap chap na juzi juzi tumeona timu ya Brigedia Charles Mbuge ilivyofanya kazi nzuri pale Dodoma, kwanini wasitumike kujenga makao makuu?
 
Kumbe kweli mganga hajigangi?!!!!!!!! wao wamejengea wenzao na kupewa sifa kem kem mpaka wamepandishwa vyeo iweje washindwe kujenga makao yao?
Labda watakuwepo pia kwenye Site ya ujenzi wakitazama mambo yanavyoenda.
 
Naelewa hayo ya ngerengere, hoja yangu ni kuwa kwanini vitu kama hivi tusijenge wenyewe? We unafahamu vizuri jeshi lilivyo mahiri katika sekta ya ujenzi. Na hii haijaanza leo nakumbuka miaka ya 80 kulikuwa na daraja la mkoloni pale old bagamoyo road lililotaka kuvunjika. Jeshi wakalijenga la muda chap chap na juzi juzi tumeona timu ya Brigedia Charles Mbuge ilivyofanya kazi nzuri pale Dodoma kwanini wasitumike kujenga?
Mganga hajigangi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda watakuwepo pia kwenye Site ya ujenzi wakitazama mambo yanavyoenda.
Sasa hapo haina mantiki, wao wamesifiwa kwa kujenga nyumba nzuri kwa bei nafuu sasa kwa nini wasijenge yao?
 
SIO KWELI. DODOMA TUNAJENGA CHUO CHA KIJESHI CHA UONGOZI KWA MSAADA WA WATU WA CHINA. SIO MAKAO MAKUU YA JESHI. NAOMBA NIRUDIE "SIO MAKAO MAKUU YA JESHI"
Hata kama ni Makao Makuu ya Jeshi kwani tatizo lipo wapi? Kwani Tanzania tuna siri gani ambayo tunaweza kuwaficha walioendelea?
 
Historia inajirudia, kila kitu tunafanyiwa, zamani na WAKOLONI(wajerumani, waarabu na waingereza) sasa na WAKOLONI(wachina, waingereza, wajerumani, US, na wengine)

Bado tumeonyesha kushindwa kutumia resources zetu vizuri na kujitegemea kwenye maeneo mengi. We're still being colonized (NEOCOLONIALISM)

1073964
 
walijenga makao makuu ya AU Adis ababa wakaweka vinasa sauti kwa siri wakawa wanadukua tu mazungumzo ndo washindwe kufanya hivyo hapo dodoma?
Tanzania tuna siri gani wewe???!!! Waache wajenge, hivi itatokea kweli Tanzania ipigane vita na China? Maadui w Tanzania ni UJINGA, MARADHI, UMASKINI, UKABILA NA UBINFSI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wana maslahi nchi nyingi,kwa mfano wadukue mazungumzo wakubwa wa jeshi wanaiongelea nchi nyingine kwa ubaya au uzuri si itakuwa rahisi kufanya hata uchonganishi?au hata kuwasikiliza kujua tu mnachokifikiria.
Tanzania tuna siri gani wewe???!!! Waache wajenge, hivi itatokea kweli Tanzania ipigane vita na China? Maadui w Tanzania ni UJINGA, MARADHI, UMASKINI, UKABILA NA UBINFSI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona hili kuhusu China Kujenga makao makuu ya Jeshi jijini Dodoma, ni kweli? Naelewa kuwa tunaushirikano na China kwa muda mrefu na hata kusaidiana katika nyanja mbalimbali lakini kwa hili kama ni kweli tutakuwa tumekosea sana.

Naomba tulijadili.


Mkuu ilitakiwa utueleze madhara/huko kukosea sana sababu ni zipi
 
walijenga makao makuu ya AU Adis ababa wakaweka vinasa sauti kwa siri wakawa wanadukua tu mazungumzo ndo washindwe kufanya hivyo hapo dodoma?

Kwa hili nchi za kiafrika tulionyesha udhaifu wa hali ya juu, yaani nchi zote 50+ tulishindwa kuchangishana wenyewe?
 
Kwani hufahamu vitu vingi vya jeshi letu vifahamika kwa wachina!!

5/5
 
Russian walijengewa jengo la Ubalozi wao na mbabe mwenzake na kukaribishwa kwa mbwembwe lakini Russians walipohamia wakagundua limefungwa vinasa sauti kila sehemu
Hili lilitokea miaka ya nyuma sana hata kama ilikuwa ni story tu lakini mataifa mengi hayakubali huu ujinga
Kama ni kujengewa lazima wataalamu wetu wawe makini sana
Ingawa hatuna utaalamu wowote wa kujua na kugundua kitu itakuwa kazi bure tu


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Makao yako Makuu ya Jeshi lako, ni kosa kujengewa na nchi au kampuni za njee. Huo mjengo ungejengwa na jeshi lenyewe, design na mainjinia wanaweza ajiriwa kutoka njee ya nchi, lakini chini ya usimamizi wa jeshi.

Somalia walijengewa makao makuu ya jeshi na Urusi, wakati wa 1977,Mrusi akawa na urafiki mzuri na Ethiopia na Somalia kwa pamoja, hawa walikuwa wahasimu wakubwa, alijaribu kuwaunganisha ilishindikana. 1977 hizi nchi mbili ziliingia kwenye mgogoro, siad Barre wa somali alikuwa mbishi, na kutowasikiliza warusi na akawafukuza. Punde somalia waliivamia Ethiopia na kuliteketeza jeshi lao na kuweza kuteka ardhi hadi Dire Dawa. Mrusi akawapa Ethopia siri za somali na pia kumshawishi Castro kupeleka majeshi ya cuba kupigana. Ndipo majeshi y somalia yalishindwa. Kama sio mrusi kuvujisha siri za jeshi la somalia mambo yangeluwa vingine.

Wamarekani na Wataliani walikuja kugundua kuwa Warusi walikuwa wakipata plani na habari zote za jeshi la somalia kupitia vifao walivyoviweka ahapo makao makuu na pia kupitia wasaliti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhamia Dodoma kunamsaidia nn mlipa kodi au kunasaidia vipi uchumi
umbali wa kwenda kufuatilia ishu za kiserikali unapungua mfano mi wa mwanza naweza kwenda dom nikafata nachofata kesho yake nikarudi sio kama dar unalazimika kuspend siku 5 kwa maana ya siku 2 kwenda bas liklala moro na siku 2 kurud bas liklala shy na siku 1 ya kushughulkia ulchokfanya
 
ila wabongo bwana? ndege vita tunanunua kwao, mitambo ya ulinzi wa anga ni ya kwao, system mbalimbali za kijeshi tunanunua kwao hivi vyote mwisho wa siku si wanaweza kuviexploit kama tutaingia kwenye shida nao? ingekua makao makuu yanajengwa na kenya, rwanda au jiran yetu yeyote ndo ingekua shida.. by the way hata hela yetu inauwa printed german na sioni kwere lolote kati yetu na german
 
Back
Top Bottom