Ni kweli Mo ni tajiri kumzidi Bakhresa?

kuna mtu alinieleza juu juu lakini nikamwelewa kidogo.

kwamba utajiri wa ssb ameugawanya kwa watoto.hauhesabiki kama wa mtu mmoja,so kama ni $1.5 igawanye mara 6,mfano azam sport club ni ya mtoto,azam marine ni ya mtoto.sasa ukichukua kwa ujumla wake bado MO hagusi.

mimi binafsi huwa naangalia hata maisha ya muhindi MO,yako kawaida sana si kiboss kulinganisha na mtoto wa bakhresa au mzee mwenyewe.angalia gari anayotumia ni ya kawaida sana.labda sababu anasimama kama msimamizi.
 
Kwa kuongezea, Azam media inamiliki media kama sita Azam sports 1&2, UTV, Azam 1&2, Sinema zetu pamoja na UFM hizi zote analipa zaidi ya million 130 kwa mwezi bado Magu hajataka vyake hapo

Bado Analipa gharama za satellite hahahahaha ni balaaa, bado analipia hizo Tv za nje ili atuonyeshe sisi mzee baba haya mambo ni magumu
 
Anamiliki Tv sita ni gharama sana yani pesa zinamtoka hatari maana kuna kodi ya gavoo, pesa ya satellite broadcasts.
Analipia huduma mbalimbali kama Channels za nje ili wewe uzione, analipia mashindano mbalimbali ili wewe uyaone huko kote anapukutika hasa!

Ndio maana sometimes anaacha kulipia maana anakuwa faida nyinyi mnabaki kulalama mechi ya Yanga katangaza itaonekana alafu anaingia mitini, Afcon ataonyesha tena bure alafu anaingia mitini hafanyi makusudi ni hela!

Azam FC hovyo ni sawa na Lipuli tu huwezi kuitaja eti nayo ni sehemu inayo mwingizia faida kubwa!

Anapopiga faida kubwa ni kwenye mabidhaa ya kula kula na kunywa kunywa huko salute
 

Hata ukiangalia kwenye hoja yangu cjajikita kwenye Tv. Tv imekuja 2013 km sikosei ila utajiri wa huyu mwamba ni toka miaka ya 80'
 
Hahaaaaa Ushaambiwa mo kawakumbatia wachina lazima wakopi siku ziende wewe unatuletetea ma power tila mjini kelele tupu
 
Napenda sana mzee Bakhressa jinsi alivyojiweka, mzee wa watu sio mtu wa kijionesha tofauti na MO. Kwa Tanzania hii Bakhressa yuko juu, MO cha mtoto.
Mo anajionesha kivipi?
 

Said Bakhressa ni Tajiri Mzee na Mohammed Dewji ni Tajiri Kijana huku tuliobaki wote tukiwa ni Masikini wa Kutupwa ila tunaowashabikia kuliko maelezo.
 
Hoja hapa sio kukopi hoja ninani tajiri zaidi ya mwenzie,alafu suala la kukopi ni suala la kawaida dunianiani .
Kuanzia makampuni ya kitekinorojia huwa yanaigana.
Mfano china ina kopi mambo mengi kutoka uingereza lakini uchumi wa china ni mkubwa zaidi ya mara nne ya uchumi wa ufaransa.
Kwa hiyo mo kumuiga bakharesa haimaanishi ya kwamba ndio kamzidi utajiri.
Mo anatengeneza bidhaa nyingi mno ambazo ni razima kwa binadamu kuzitumia katika maisha ya kila siku.
Mfano Tambi,sabuni za kufuria na kuogea,mafuta ya kupikia ,viberiti.
Alafu unapo sema eti tambi za mo ni mbaya ni kwa mtazamo wako, kanda ya ziwa yote tambi za mo ndizo zinanuliwa sana kuliko nyingine.
Hata huku kahama ninapo kaa bidhaa za mo ndizo zimetawala soko kuanzia vinywaji baridi,unga,mafuta ya kupikia,sabuni,tambi.
 
Je kama ni kweli itakusaidia nini wewe?
Kaoshe masufuria dadako karibu anatoka saluni na shemeji yako yuko njiani
 
Hata ukiangalia kwenye hoja yangu cjajikita kwenye Tv. Tv imekuja 2013 km sikosei ila utajiri wa huyu mwamba ni toka miaka ya 80'
Mo ni mjanja sana viwanda vyake vingi haviko Bongo kawekeza nchi nyingine za Afrika kama Zambia, Mauritius n.k.

Bongo nyoso kodi ni za kufa mtu japo sikatai ile familia ina pesa ila wanagawana sana na serikali
 
Mo anamiliko 75pc ya METL, Azam subsidiaries nyingi zinamilikiwa na watoto wake. Hivyo inakuwa ngumu sana kujua nani ni zaidi ya nani.
Ukiwaweka METL na Kampuni zote za Azam Azam anawazidi METL kwa turnover. ...

Hakuna ugunduzi mpya duniani. Unachukua cha mwenzako unamodifiy ili kuondoa monopoly
 
Watu wanatengeneza bidhaa sawa na kampuni nyingine ili waondoe monopoly. Hebu fikiria soda angetengeneza Azam pekee yake.
Tz ingekuwa na chanel moja tu
Tz ingekuwa na kiwanda kimoja tu cha maziwa
Kiwanda 1 tu cha ngano


Tuache chuki, ushindani wao ndo nafuu kwetu kuchagua tununue wapi na kwa bei gani
 
Jamani utajili sio kama makalio.huyu mnyaturu hana lolote zaidi ya blabla tu .20b .pale simba Sc.wanazisikia tu.Uwanja wa Bunju nao ni Stori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…