Gwajima
JF-Expert Member
- Sep 6, 2018
- 253
- 406
Siku chache kabla ya kutenguliwa kwa uteuzi wa ndugu Faustine Ndugulile na Merdad Kalemani, tulishuhudia Wizara zao zikiingia makubaliano ambapo TANESCO walikubali kutumia miundombinu yao kusambaza mkongo wa taifa majumbani ili kuwezesha wananchi kupata huduma za internet, simu na Tv kwa gharama nafuu.
Kuna tetesi kuwa makubaliano haya yaliwakera sana matajiri wanaomiliki makampuni ya mawasiliano kwani huenda wangepunguza wateja wao, pia inaelezwa kuwa watoa huduma za visimbuzi nao hawakupenda mradi huu hivyo wakawasemea kwa mama kuwa mradi huu utapunguza wawekezaji na mama bila ajizi akawapumzisha.
Sijui kama ni tetesi tu au ndivyo ilivyo, nataka Serikali iseme kama mradi huu utaendelea au hautafanyuka, endapo hautafanyika basi tetesi hizi zitanishawishi, kama utafanyika basi mnaonena chini chini mkome kuzusha mambo.