Jamaa anamletea PW Wireless Mic katika stand (Pengine ilikuwa na sumu Tayari) Baada ya Muda Jamaa yuleyule anakuja na Kuchukua ile Mic na kutokomea nayo (Pengine alihisi sumu haitoshi akaenda kuongezea Dose) Jamaa anakuja na Mic ikiwa Vilevile kwenye stand, Anamwekea PW, halafu anaondoka kuelekea alikotoka. Muda Mfupi PW anaanguka ghafla, Watu wanamzunguka kusaidia. Jamaa yuleyule anatokeza tena. Cha kwanza Badala hata ya Kushangaa, au hata kwa Udaku tu kuinama na Kujua PW yupo katika hali gani, Yeye Bila Kustushwa anachukua Mic ile tena, Anasogea Kidogo, anacheki Noma! Kisha anatokomea Nayo. Mwanzo Unaweza Kusema Kuwa labda Kuisogeza Mic Pembeni ni sawa ili Kupisha watu Kumsaidia PW, Lakini Lengo lake linaonekana wazi, Anachukua Mic na Kuondoka Bila Kujali au Kushangaa aliyeanguka kimempata Nini au yu hali gani. Ungedhani Mtu anayehangaika na Mics awe mhudumu na angekuwa mstari wa Mbele kusaidia. Huyu Hakuwa Ndiye "Hit Man"