Ntozi
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 226
- 300
Hizo b 100 una hakika zilitolewa mkuu?Siasa na sihasa labda.Kati ya Jambo linaloshangaza wengi hadi sasa ni kitendo cha serikali kushindwa kujua kuwa billion 100 isingekuwa Suluhu la ongezeko kubwa la bei ya mafuta ya petrol na dizeli.
Watanzania wengi wasiolewa mambo walidhani kuwa ikiweka billion 100 basi kila kitu kuanzia mafuta na bidhaa zingine zitakuwa nafuu au baadae zitakuwa nafuu lakini ukweli ni kwamba hali inaonesha wazi kuwa mafuta yataendelea kupanda na bidhaa zitaendelea kupanda!
Ni nani aliyemshauri na kumshawishi Rais Samia kuwa billion 100 ruzuku itakuwa suluhu na si kuondoa mlolongo wa tozo zilizopo kwenye mafuta?
Hivi Rais Samia na washauri wake kwanini hawakufikiri kwamba kupunguza mlolongo wa tozo zilizo jaa kwenye uingizaji wa mafuta inaweza kuwa suluhu kubwa kuliko kuchukua billion 100 pesa za walipa kodi na kuzipoteza bure?
Kuna ugumu gani kupunguza au kuondoa tozo za mashirika zaidi ya kumi kwenye mafuta?
Hivi kuwambia watanzania mafuta yamepungua kwa Tsh 150 si ni kuwatania na kuwafanya wajinga?
Kwanini tumetekeza billion 100 na hazijaleta suluhu yeyote?
Bidhaa zote zimepanda bei na zinapanda kila siku na hata bidhaa za stationary na ujenzi zinazidi kupanda na kila mtu anasema shida ni kupanda kwa mafuta!
Hii Tsh 150 itasababisha kushuka kwa nauli na hizo bidhaa? Kwanini tumepoteza tena billion 100 bila sababu?