AKILI TATU
JF-Expert Member
- Feb 10, 2016
- 2,659
- 2,827
Itakuwa ni kituko cha karne kuamini timu yenye wanachama hai zaidi ya 5000 na mashabiki wa kutosha zaidi ya milioni 10 ,yenye mali nyingi za kutosha (pamoja na kwamba hazithaminiki) yenye historia ya Soka la Tz kwa naman ya kipekee leo hii eti inathaminishwa na dau dogo kiasi hiki?
Hivi viongozi wa simba waliopoa na waliopita wameshindwa kuifanya simba kutengeneza bilioni 20 zao kwa kuitumia LOGO ya klabu hiyo vizuri kibiashara?
Hivi ni kweli simba imeshindwa au inashindwa kujua thamnai yake miongoni mwa mashabiki wa soka afrika? ni nani asiyejua kuwa Simba ni moja ya timu zinazokubalika sana katika ukanda huu wa afrika mashariki? nenda Uganda,Kenya hata Burundi kote huko utakuta simba inamashabiki wengi tu,usisahau falme za uarabuni,ulaya na marekani.
Je Simba imeshindwa kabisa kabisa hata kuuza peni na pipi tu zenye nembo ya kbalu hiyo ili waitengeneze hiyo bilioni 20 ya Mo dewji ndani ya msimu mmoja?
Ni kweli kabisa kabisa Simba yenye jengo lenye thamani ya bilioni 2 hadi tano katikati ya mji leo hii inahitaji uwekezaji wa bilioni 20 tena uwekezaji wa kudumu?
Simba wameshindwa kuitumia hata NSSF na mashirika mengine ya fedha kuingia nao mkataba wa miaka walau 10 ya ukarabati wa jengo lao au uwanja wao hata uzungushiwe mabati tu ?
Simba ni kweli kabisa kabisa mnadiriki kushupalia Mo ainunue klabu hiyo moja kwa moja? hivi mnajua athari zake huko mbeleni?
Moja ya athari ni pamoja na timu kuaj kuuzwa kwa watu wasio na mapenzi na klabu hiyo matokeo yake ni kuishuhudia timu ikitua mikonni mwa wachache wasiokuwa na uwezo wa kuiendesha au wasio jali muda wa kuiangalia matokeo yake timu ni kuyumba na kufa kabisa.
Simba kama kuna kosa ambalo mtalifanya ni kukubali Mo Dewji aichukue simba hii iliyotaabani kisha na kuipa dawa ya kutuliza ugonjwa madala ya kuipa dawa ya kuiponya ,binafsi yangu naamini kabisa ipo siku MO ataiuza simba ,na mtu atakaye nunua atainunua kwa daiu dogo ,kitu ambacho kitasababisha timu kushikiliwa na watu HEWA.
Viongozi wa simba ni vema mkatafakari,Bilioni 20 za Mo dewji zisiwababaishe hiyo ni pesa ndogo sana kulingana na thamani halisi ya klabu ya Simba,hiyo pesa haitoshi hata kuifanya klabu ijiendeshe yenyewe kwa miaka mitano.
Simba ya mashabiki milioni 10 na wanachaam 5000 haiihitaji mtu kama Mo kuja kuwekeza tupesa tudogo kiasi hiko,hiyo pesa Simba wakiamua kuipata wanaipata kiurahisi sana kwa kutumia watu walioelemika na wabunifu wa masuala hayo.
Simba iamue sasa,timu kama Newcastle,astoni vill ana nyingine nyingi zinatamani kuwa ufalme wao katika nchi kama tanzania