Ni kweli Simba ina thamani ya bilioni 20?

Ni kweli Simba ina thamani ya bilioni 20?

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
2,659
Reaction score
2,827
Itakuwa ni kituko cha karne kuamini timu yenye wanachama hai zaidi ya 5000 na mashabiki wa kutosha zaidi ya milioni 10 ,yenye mali nyingi za kutosha (pamoja na kwamba hazithaminiki) yenye historia ya Soka la Tz kwa naman ya kipekee leo hii eti inathaminishwa na dau dogo kiasi hiki?

Hivi viongozi wa simba waliopoa na waliopita wameshindwa kuifanya simba kutengeneza bilioni 20 zao kwa kuitumia LOGO ya klabu hiyo vizuri kibiashara?

Hivi ni kweli simba imeshindwa au inashindwa kujua thamnai yake miongoni mwa mashabiki wa soka afrika? ni nani asiyejua kuwa Simba ni moja ya timu zinazokubalika sana katika ukanda huu wa afrika mashariki? nenda Uganda,Kenya hata Burundi kote huko utakuta simba inamashabiki wengi tu,usisahau falme za uarabuni,ulaya na marekani.

Je Simba imeshindwa kabisa kabisa hata kuuza peni na pipi tu zenye nembo ya kbalu hiyo ili waitengeneze hiyo bilioni 20 ya Mo dewji ndani ya msimu mmoja?

Ni kweli kabisa kabisa Simba yenye jengo lenye thamani ya bilioni 2 hadi tano katikati ya mji leo hii inahitaji uwekezaji wa bilioni 20 tena uwekezaji wa kudumu?

Simba wameshindwa kuitumia hata NSSF na mashirika mengine ya fedha kuingia nao mkataba wa miaka walau 10 ya ukarabati wa jengo lao au uwanja wao hata uzungushiwe mabati tu ?

Simba ni kweli kabisa kabisa mnadiriki kushupalia Mo ainunue klabu hiyo moja kwa moja? hivi mnajua athari zake huko mbeleni?

Moja ya athari ni pamoja na timu kuaj kuuzwa kwa watu wasio na mapenzi na klabu hiyo matokeo yake ni kuishuhudia timu ikitua mikonni mwa wachache wasiokuwa na uwezo wa kuiendesha au wasio jali muda wa kuiangalia matokeo yake timu ni kuyumba na kufa kabisa.

Simba kama kuna kosa ambalo mtalifanya ni kukubali Mo Dewji aichukue simba hii iliyotaabani kisha na kuipa dawa ya kutuliza ugonjwa madala ya kuipa dawa ya kuiponya ,binafsi yangu naamini kabisa ipo siku MO ataiuza simba ,na mtu atakaye nunua atainunua kwa daiu dogo ,kitu ambacho kitasababisha timu kushikiliwa na watu HEWA.

Viongozi wa simba ni vema mkatafakari,Bilioni 20 za Mo dewji zisiwababaishe hiyo ni pesa ndogo sana kulingana na thamani halisi ya klabu ya Simba,hiyo pesa haitoshi hata kuifanya klabu ijiendeshe yenyewe kwa miaka mitano.

Simba ya mashabiki milioni 10 na wanachaam 5000 haiihitaji mtu kama Mo kuja kuwekeza tupesa tudogo kiasi hiko,hiyo pesa Simba wakiamua kuipata wanaipata kiurahisi sana kwa kutumia watu walioelemika na wabunifu wa masuala hayo.

Simba iamue sasa,timu kama Newcastle,astoni vill ana nyingine nyingi zinatamani kuwa ufalme wao katika nchi kama tanzania
 
Mkuu hujaelewa nadhani, nenda ktk mkuu utaelewesha mo hataki kuinunua simba, ila timu inatoka ktk mfumo wa umiliki wa wanachama kwenda ktk mfumo wa hisa, so sio mo tu ata wew utaruhusiwa kwenda kuwekeza kwa kuwa na hisa zako kwahyo kaa ukijua simba haiuzwi ila itakuwa na umiliki wa mfumo wa hisa
 
Huu ni uchawi dhidi ya maendeleo ya soka la bongo,,mmekaa nayo club zaid miaka 80 mmeshindwa kutuonesha ni namna gani tunaweza kuzalisha billion 1 kwa mcm ,anakuja MTU mfanyabiashara nguli anaweka mzigo wa kutosha still anapigwa majungu,wabongo tunataka nini??
 
Ni wanasimba wachache sana watakao muelewa bilionea mo.
Malengo ya mo hayataeleweka nikama kumchukuwa prof kwenda kufundisha chekechea.
Mo anaona mbali sana na anamalengo ya muda mrefu na ya maana na kibiashara yenye maslahi na simba na biashara zake.
Lakini kuna vijitu pale binauza fulana za simba wanapata kula yao na familia zao wataanzisha maneno yasio kuwepo kwa kukwamisha malengo mema ya mo.
 
thamani ya simba ni zaidi ya hizo psa kichekesho mo anakuja na bei yake kabisa mara nyinga kama mtu anataka kununua kitu kwako muuzaji ndio anapanga bei huyu mo anatumia wanachama njaa na waandishi njaa kutaka kununua simba kama kweli ana mapenzi afanye udhamini kipindi anaidhamini simba alikuwa anaitumia kutangaza bidhaa zake wanachama amkeni
 
Ni wanasimba wachache sana watakao muelewa bilionea mo.
Malengo ya mo hayataeleweka nikama kumchukuwa prof kwenda kufundisha chekechea.
Mo anaona mbali sana na anamalengo ya muda mrefu na ya maana na kibiashara yenye maslahi na simba na biashara zake.
Lakini kuna vijitu pale binauza fulana za simba wanapata kula yao na familia zao wataanzisha maneno yasio kuwepo kwa kukwamisha malengo mema ya mo.
Mwanafalsalfa, Albert Einstein alishawahi kunena.. "If you can't explain to a six-year-old, you don't understand it yourself".

Sasa kama Mo anashindwa kutuelewesha lengo lake ni nini hasa.. Ina maana hata mwenyewe hajui anachotaka kukifanya.
 
kwa hiyo wewe unaridhika na hali ya simba kuongozwa kizamani tu na wanacham?miaka themanini bila hata uwanja wa mazoezi?acha porojo acha simba iwe kampuni iende kisasa zaidi au wewe ni mtoto wa wale wanaonufaika milangoni na kuishi dar kwa mgongo wa club?
 
mnataka kila siku mupitishe bakuli michango kuisaidia club dah!kweli wabongo ni masikini wa mawazo hata hili nalo linapata wapinzani dah!kuzaliwa tanzania ni mikosi kwa kweli duuh!watu hawaoni na hata kufikiria shida?eti simba inathamani kubwa!iko wapo thamani hiyo karne moja hatuna hata hostel za wachezaji?usajili tunategemea akina hans pop!
 
Mkuu hata Ac Milan inter Milan hawana uwanja wao..... Timu nyingi Italia hazina viwanja Juve ndio kamaliza juzi juzi tu ndio maana anawasumbua wenzake..... Fact ya uwanja sio lazima
kwa hiyo wewe unaridhika na hali ya simba kuongozwa kizamani tu na wanacham?miaka themanini bila hata uwanja wa mazoezi?acha porojo acha simba iwe kampuni iende kisasa zaidi au wewe ni mtoto wa wale wanaonufaika milangoni na kuishi dar kwa mgongo wa club?
 
kwani club ikinunuliwa wanachama wanahama?au kuondoka mo kasema bado wanachama watapewa hisa bue!ndg yangu acha tubadili mfumo tuone uoga ni mbaya sana club haina vision ile kwa sasa tutachagua na kubadilisha viongozi kila mwaka club haisogei! kama simba ikibaki vile hata tufanyeje hatuwezi kupata ubingwa kwani azam na ndg zetu yanga wametulia sana unadhani kwa nini yanga wamemwacha manji muda wote huo?machungu ya yanga ni tofauti na machungu ya simba kwa sasa! acheni club ibadili mfumo nasisi tupate hisa!
 
thamani ya simba ni zaidi ya hizo psa kichekesho mo anakuja na bei yake kabisa mara nyinga kama mtu anataka kununua kitu kwako muuzaji ndio anapanga bei huyu mo anatumia wanachama njaa na waandishi njaa kutaka kununua simba kama kweli ana mapenzi afanye udhamini kipindi anaidhamini simba alikuwa anaitumia kutangaza bidhaa zake wanachama amkeni
Huu tunaita uchuro tu, miaka yote hiyo wewe ulikuwa wapi?
 
Nitalia na simba had I kesho naona simba inatoka kwa masikini wa kitanzania walioifikisha hapa kwa raha na shida na kuipeleka kwa matajiri ambao hata mpira hawajui
 
Unajua watu tunashindwa kulewa Mo kaeleza vzur mpango ake ila watu bado hawajamuelewa kaeleza hzo 20 bill anazotaka kuwekeza kwa simba sc kwamba anawapa viongozi ila itakua ataikopesha serikal na kila mwaka simba itakua inapata gawio la billion tank kama faida na hizo ndizo zitakazotumika kwa ajili ya maandalizi ya timu kupitia tressure bond, na alichokisema no ni kubadli mfumo tu wa uendeshaji wa club kwa mfumo wa hisa na kaeleza waz kilamwanachama anayo haki ya kuimiliki club ya simba na wale wanachama wa muda mrefu kaeleza wapewe hisa bure ili wacionekane kutengwa hapo ndio patamu, we ulie sema simba haina thaman ya 20 bill je simba kwa mwaka inazalisha kiasi gan cha pesa? Na vyanzo vya mapato vya simba no vp? Laiti laiti kama viongozi wa club zetu za mpira wangekua na jicho la kibiashara wangefika mbali mno wangeweza kutumia mtaji wa mashabiki wao na wanachama na hatawapenzi wengine wa vilabu vyao kujitengenezea kipato ila WAP, Leo amekuja mtu .wenyejicho la biashara tunamuona anataka kuihujumu timu, haya maamuzi in yakwetu wenyewe. Ila mi najua wanaopinga hili suala no wapigaji tu.
 
kitu ambacho mnapawa kukielewa wakuu,Simba hii ya sasa ,Jina lake tu kibiashara linathamani ya hiyo pesa,twende mbele turudi nyuma wanachama wa simba na mashabiki wa simba wengi wenu mnapelekeshwa na kivuli cha utajiri wa Mo Dewji,sawa sikatai kuingia katika mfumo huo,lakini iwe kwa thamani halisi ya klabu,Simba ni mgodi unaotemea uliotelekezwa umekosa wachimbaji wa kuchimba madini yaliyopo,narudia tena Logo pekee ya simba ikitumika vizuri kwa mwaka inaingiza zaidi ya hizo pesa,tamasha la Simba day likiandaliwa vizuri linaweza kuingiza si chini ya 2 bilioni kwa kila mwaka,bado ada za wanachama ,vitega uchumi ikiwemo majengo yale mawili yote kwa thamani huenda yakaifka zaidi ya bilion za pesa ,Simba inautajiri ambao umeshindwa kuinuifaisha yenyewe,leo hii ukisema uje kwenye upande wa hizo hisa kulingana na thamani ya simba pengine hisa moja ya simba ingeweza kuuzwa si chini ya tsh 10000 kwa kila hisa.

Sawa anainunua kwa mtindo wa hisa je ni sahihi yeye kujipangia bei? hapa ndio panadhihirisha kuwa Simba na wanasimba wake NI SAWA na ule usemi wa penye udhia penyeza rupia?

Kwa nini Simba wasingepanga bei wao wenyewe,au wakatangaza kuuza hisa kisha hao matajiri wakajitokeza kununua?

Mwisho wa siku Simba itabaki kuwa ni ya wanasimba ,kama ni hivyo je siku ikitokea Mo akaamua kuuza hisa zake zote kwa tajiri mwingine ambaye haifahamu Simba na hana mapenzi ya kweli na Simba unadhani kuna ambacho kitafanyika?
 
Huu ni uchawi dhidi ya maendeleo ya soka la bongo,,mmekaa nayo club zaid miaka 80 mmeshindwa kutuonesha ni namna gani tunaweza kuzalisha billion 1 kwa mcm ,anakuja MTU mfanyabiashara nguli anaweka mzigo wa kutosha still anapigwa majungu,wabongo tunataka nini??
Kujifanya kujua, kumbe tunaungua jua. Maneno Mengiiiii
 
thamani ya simba ni zaidi ya hizo psa kichekesho mo anakuja na bei yake kabisa mara nyinga kama mtu anataka kununua kitu kwako muuzaji ndio anapanga bei huyu mo anatumia wanachama njaa na waandishi njaa kutaka kununua simba kama kweli ana mapenzi afanye udhamini kipindi anaidhamini simba alikuwa anaitumia kutangaza bidhaa zake wanachama amkeni
Hata hiyo 20 b ni nyingi sana thanani ya timu inapatikana kwa timu kuchukuwa makombe bila kuchukuwa makombe timu haina thani.
Angalia leo hii timu zipi zinathamani ktk bora huko ulaya kwa na zipi hazipa thamani.
Miakaya 70 mpaka thamani timu kama man u ilikuwa haina thamani kwakuwa ilikuwa haichukuwi makombe leo man u ndio timu yenye thamani kubwa.
Acheni mo atengeneze timu ya ushindi na ya kisasa muhim ni mikataba imara na mizuri tu kwa maslahi ya klabu.
Hii sio dunia tena ya mpira wa kutegemea wachawi na kuhonga.
 
Achen wehu nyie embu mtupe bas thaman ya team ya simba na sio kulia Lia hapa et simba doesn't worth 20bln
Kwanza naona mo Ame take very big risk kuweka hela zake kwa team kama ya simba especially kama kuna watu wana mawazo kama ya kwako!
Kabla hujasema 20bln ndogo bas mtuambie simba ina thaman kias gan na vitu gan vya kufikisha hyo thaman
Achen na story za pip na big kwa maana hakuna kitu kama hicho mtupe real facts
 
Back
Top Bottom