Ni kweli Tanzania inabana Matumizi kama viongozi wake wanavyodai?

Taeyong

Senior Member
Joined
Sep 29, 2019
Posts
160
Reaction score
206
Salaam wana JF,

Niende direct kwenye point. Tanzania imepeleka watu 736 katika mkutano wa mabadiliko tabia ya nchi huko Dubai #Cop28

Msafara ambao unajumiasha viongozi,wafanyabiashara,makatibu,wasaidizi nk.. Je nani anagharamia tiketi? Maradhi? Posho? Za kwenda na kurudi mpaka mkutano huo utakapokua umekwisha za wajumbe wote kwa taifa ambalo tunakopa kila kukicha !? Nina maswali mengi emu tuanzie hapo kwanza.

Kuangalia orodha ya majina ya wajumbe wote wa msafara fungua link 👉🏿 Mwango Capital: List of Tanzanian Attendees of COP 28

Nakaribiisha maoni.
 
Wanabana matumizi ya pesa zao binafsi ili waweze kula na kusaza kifisadi pesa za maskini wanaokamuliwa kodi.
 
Hakika, kama taifa bado tuna safari ndefu sana kuja kupata wazelendo wa kweli kwa taifa hili.
 
Siku zote kwenye mambo ya kipumbavupumbavu yanayowahusu wao hela zipo ila ya maana yanayowahusu wananchi wengi hela hamna
Nchi ngumu imagine hao watu wote kuwalipia hotel, tiketi,vyakula na posho🙌🏿
 
Inaonekana kuwa ndege tunazonunua hazina route zinazoweza kurudisha gharama za uwekezaji.

Sio ajabu mwakani tukamsikia CAG akitoa tathmini ya Air Tanzania kujiendesha kwa hasara kwa kutegemea zaidi tenda za Serikali hasa kwenye safari za Rais na ujumbe wake.

Air Tanzania itakuwa na abiria wachache sana wanaosafiri kwenda India kwa Airbus 220-300 wakati Boeing 737-9 ikiwa imepaki Dubaï kusubiri wajumbe wa mkutano wa mazingira.....Matumizi mabaya ya pesa za umma kwa kiwango hiki yanaweza kutafsiriwa kama uhujumu uchumi kwa makusudi au kutokujali.
 
Hebu tuanze kuwa lama wenzetu na kufanya wenyewe kwa kuchanga hela na kufungua charity tuiite jf charity
Huu umasikini hautaisha labda tubadilike bila kuitegemea serikali sana
Hata wenzetu wana Charities za kila aina na kila leo wanachanga ili kwenye shida wasaidie
Misaada yao kwa wananchi ni mingi sana mpaka mingine kwa roho zao za huruma wanaamua kuwaletea na nyie

Kweli hii shule mtasema ni ya karne hii? Hebu tuanze kwa kusaidia ingawa hatuna utamaduni huo, ila kama mnataka mabadiliko ndio haya
Mloenda Ocean Road mbana mkaishia huko kwa safari mbili tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…