Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Kila mtihani wa taifa kunakuwa na route za misafara ambapo kila ruti ina watu hawa;

(A) wasimamizi wakuu wa mitihani (supervisors- ambapo mara nyingi ni maafisa wa elimu )
(B) wasimamizi wa ndani wa mitihani (invigilators- yaani walimu)
(C) watu wa ulinzi wa mitihani (polisi na migambo)
(D) watu wa usalama wa mitihani (maafisa/watu kutoka ofisi ya usalama wa taifa)

Kulingana na utaratibu huo kwa wale wakongwe kwenye maswala ya usimamizi wa mitihani ya kitaifa imekuwa ni rahisi kwao kuwajua/kujuana wao kwa wao

Juzi kwenye mapokezi ya mwenge sasa kabla ya mwenge kufika sehemu ile ghafla ikaja gari na wakashuka watu kadhaa ambao kwa haraka haraka watatu waligundulika kuwa ni walewale ambao huwa wanakwepo kwenye mitihani kwa utambulisho wa kundi D. Walivalia locally tu kama kawaida yao, wakazunguka zunguka tu pale wakikagua kisha baada ya muda hao wakasepa kisha jioni ndipo mwenge ukafika pale

Sijui tu hata nimeandika nini hebu aliyeelewa anisaidie maana me mwenyewe sielewi
 
Wanafahamiana kama wako kwenye mishe moja ila kama hawako mishe moja hawajuani

Na kama wamekutana mazingira anaweza kuhisi kwa kuona tabia za mwenzake sijui nimeeleweka maana hata mwenyewe sijaelewa nilicho kiandika
 
Wanafahamiana kama wako kwenye mishe moja ila kama hawako mishe moja hawajuani

Na kama wamekutana mazingira anaweza kuhisi kwa kuona tabia za mwenzake sijui nimeeleweka maana hata mwenyewe sijaelewa nilicho kiandika
Hawanaga depo?
 
Wapo kila sehemu Airport, Tanesco sijui bandarini kila sehemu wapo kwenye mashirika ya serikali mpaka private sema taarifa wanazozipenda watawala nizile kama wanahatarisha utawala wao lakini kwenye kila kitengo wapo tena wengi tu. Taarifa zao zinafanyiwa kazi inategemea na kiongozi anataka kujuwa nini shida viongozi wamejikita kwenye usalama wao sio upigaji ila kama wako serious kabla ya report ya CAG wanajuwa kila upigaji.
 
Ikulu ya dodoma! Geti la kwanza,la pili na la tatu! Endelea tu kutoa Siri za hapo!!
 
Mkuu
Bado najiuliza, lengo la kuwafahamu hao TISS ni nini haswa?

Kama wapo na kama sheria inataka wasiwe public known basi tuache hiyo kwa sababu kuwafahamu ni kama kujianika usalama wetu ulivyo na adui anajipanga apenye wapi.

Nchi zinazozingatia uhai wa Taifa lao, hakuna utamaduni kama huu wetu wa kujimwambafai kuwa unajuana na TISS au yule ni TISS (kwa mataifa hayo)

Tanzania tuna mbwembwe nyingi asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…