Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Wanabodi, weekend hiyooo na kamvua kwa mbali hapa Arusha!

Nipo Triple A hapa. Kuna jamaa yangu ananiambia eti wana usalama/TISS hawafahamiani na hawaaminiani kabisa!

Yaani kila mmoja ana majukumu yake na mahala pa kureport. Hawana mazoea ya mwenzangu uko wapi, unafanya nini!

Hawaaminiani, hawajuani kivile!

Hii kitu ni kweli au ni mfumo kama tu wa TAMISEMI au taasisi zingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo wanaofahamiana, lakiki pia wapo wasiofahamiana.
Aidha, ni kweli kwamba hawaaminiani, ndio maana wao kwa wao wanachunguzana kwa Siri bila kujuana wao kwa wao.
 
Kuna wanaojuana, kuna wasiojuana, kuna wanao-wafanyia ujasusi wenzao uku nao wakifanyiwa ujasusi bila kuwajua wanaowafanyia ujasusi, kuna wanaofanyishwa kazi za usalama bila wao kujijua, iwe kwenye siasa, biashara, dini kote wapo majasusi.

Tatizo la ujasusi wa bongo umejikita kwenye kukusanya taarifa zaidi za mambo mbali mbali kusaidia utawala uliopo madarakani tofauti na wenzetu ambao wanajikita sana kwenye kuzuia hatari zote mbaya zizazohusu uchumi na siasa bila kuegemea upande wowote wa kisiasa.

TISS wanatakiwa kujikita kwenye ujasusi wa kiuchumi jinsi ya kutengeneza mabilionea, jinsi ya kupigana vita ya kiuchumi na mataifa jirani, kuhakikisha taarifa za kiujasusi wanazokusanya zinafanyiwa kazi haraka bila kuegemea upande wowote.
Hapo inatakiwa mtu talented, hawa wa kwetu naona wengi hawapatikani kiushindani!
 
Hii kuhisiwa kuwa mimi Usalama huwa sipendi kabisa! kwa muda mrefu hii hali inanitesa! maneno yanazunguuka hadi yananikuta mimi mwenyewe tuhuma za kilofa kabisa!
 
Hii kuhisiwa kuwa mimi Usalama huwa sipendi kabisa! kwa muda mrefu hii hali inanitesa! maneno yanazunguuka hadi yananikuta mimi mwenyewe tuhuma za kilofa kabisa!
Wapi huko wanakuhisi kazini au mtaani?

Au wewe ndio unajihisi boss
 
Wanabodi, weekend hiyooo na kamvua kwa mbali hapa Arusha!

Nipo Triple A hapa. Kuna jamaa yangu ananiambia eti wana usalama/TISS hawafahamiani na hawaaminiani kabisa!

Yaani kila mmoja ana majukumu yake na mahala pa kureport. Hawana mazoea ya mwenzangu uko wapi, unafanya nini!

Hawaaminiani, hawajuani kivile!

Hii kitu ni kweli au ni mfumo kama tu wa TAMISEMI au taasisi zingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawawezi kuaminiana maana saa zingine wanatumwa kumalizana wao kwa wao kwa wale waliokiuka maagizo ya wakuu wao.
 
Kwani huku kwetu wanapatikanaje boss?
Sio kwa ubaya ila kuna kitu nimekinotice kwako. Hii I'd yako ni mpya hapa jf ila nyuzi ulizochangia ni zinahusu Tiss au majeshi tu tena kwa vimaswali chokonozi.
Screenshot_20231219_084826_com.android.chrome.jpg
 
Sio kwa ubaya ila kuna kitu nimekinotice kwako. Hii I'd yako ni mpya hapa jf ila nyuzi ulizochangia ni zinahusu Tiss au majeshi tu tena kwa vimaswali chokonozi.View attachment 2846805
Kumbe na wewe umemshitukia eeh!? Nilidhani ni Mimi peke yangu niliyeona hili.Hao ni miongoni mwa 'watu wao wengi' waliotumwa huku kwenye mitandao ya kijamii ili kuwafuatilia watu kwamba wanasema nini kuhusu wao, pamoja na kufanya online surveillance dhidi ya targets zao Fulani Fulani hapa mtandaoni au ku-disrupt mijadala pevu mitandaoni inayokosoa au kuibana idara yao.
 
Ilikuwa ni wakati wa jk nyerere lakini siku hizi wanatiana hadi mimba
 
Back
Top Bottom