Ni kweli tuidai Serikali maji, au tudai sheria ya kuhifadhi vyanzo vya maji?

Ni kweli tuidai Serikali maji, au tudai sheria ya kuhifadhi vyanzo vya maji?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Bunge litunge sheria kali ya kutunza mazingira. Baada ya sheria kali ya money laundering ambayo haina dhamana, basi ninatamani Bunge lije na sheria kali ya mazingira. Ninadhani bado sheria ya mazingira tuliyonayo haijakidhi haja au imeshindwa kusimamiwa.


Udhaifu wa usimamizi au ubutu wa sheria ndiyo unaoleta malalamiko kuwa serikali haiwapelekei watu maji. Kama sheria ya mazingira ingesimamiwa vizuri Tanzania maji isingekuwa tatizo, maji safi isingekuwa tatizo bali tatizo ingekuwa maji salama. Kwa mfano mito mingi sasa inakauka hii ni kwa sababu kuna kilimo holela kwenye vyanzo vya maji, kuna ukataji wa miti hovyo. Unapokata miti ambayo ndiyo kichocheo cha uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa maji unajitengenezea bomu la kukosa maji.


Hasara ya vyanzo asilia vya maji kukauka ni nyingi. Mojawapo ni wananchi kukosa maji yetu ya asili yanayotiririka na kukosa pia maji ya bomba. Maji ya bomba hukosekanika kwa kuwa serikali inahitaji kutumia fedha nyingi kuvuta maji wakati mito ya asili ingekuwepo serikali ingetumia pesa kidogo kuwaletea wananchi maji. Maeneo mengi nchini ukipita unaishia kuona makorongo ambayo zamani kulikuwa na maji lakini kwa sasa yalishakauka. Yapo maeneo ambayo miaka kumi iliyopita tulifuata maji mita 500 tu kuchota maji mtoni, lakini kipindi wananchi hawa hawa wanalazimika kufuata maji ya mtoni zaidi ya KM 3 kwa kuwa mto waliokuwa wanachota maji kwa kutembea mita 500 tu ilishakauka kwa sababu ya kutokutunza vizuri mazingira.


Maji ni uhai, binadamu hawezi kuishi bila maji. Ninadhani tunawajibu wa kutunza vyanzo vyetu vya maji vilivyopo kabla ya kudai maji salama ya bomba serikalini hasa kwetu sisi wa vijijini. Ninatamani uharibifu wa mazingira hasa ukataji hovyo wa miti, kilimo holela na ufugaji hovyo ni chanson kikubwa cha kuhatarisha uharibifu wa mazingira ambayo matokeo yake ndiyo huku kukosa maji. Kama sheria zipo basi kunauzembe mkubwa kwa viongozi wa serikali za mitaa ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa sheria hizi. Tusimsubirie hili nalo RAIS alisemee. Wakurugenzi, Watendaji wa kata na vijiji wanayonafasi ya kusimamiwa hili.


Mwisho wataalamu wa Tanzania njooni na mkakati wa kuvuna maji ya mvua. Tanzania Mungu ametujalia mvua nyingi, lakini wataalamu hawajaja na mkakati wa kuvuna maji ya mvua ambayo yanaweza kulisaidia Taifa na Watanzania wengine kuondokana na changamoto ya maji hasa kwa mikoa ya Dodoma, Tabora, Singida na maeneo ya Manyara. Huu ni Ushauri Wangu ninadhani wajuvi wa Mambo mtaniongezea maarifa kwa kuchangia uzi huu.
 
Back
Top Bottom