Ni kweli uchawi hauwezi "kuvuka" maji?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kipindi fulani, nikiwa ninafanyia shughuli zangu maeneo ya machimbo ya dhahabu, nilifahamiana na kijana mmoja kutoka mkoani Kigoma. Alikuwa anafanya vibarua machimboni.

Kuna wakati alinifuata kwa ajili ya kuniomba ushauri. Aliniambia kuwa alikuja machimboni kama njia ya kumtoroka babu yake aliyekuwa akitaka kumridhisha uchawi. Japo kwa maelezo yake aliniambia kuwa alishawahi kushiriki kwenye matukio ya kichwawi, tena kipindi angali shule ya Msingi, kwa kipindi hicho alikuwa ameshaachana na hiyo tabia. Aliniambia alikuwa ameamua kuwa Mkristo. (Hata hivyo sikumwamini sana kama kweli alikuwa Mkristo kutokana na baadhi ya matukio aliyonisimulia na niliyoyashuhudia kwake).

Siku moja akiwa amelala kambini na wenzake, aliamka Usiku wa manane akaenda nje. Kitendo cha kutoka tu nje, alimkuta babu yake kajiinamia akiwa amejifunika vazi kama shuka au blanketi hivi.

Akiwa katika hali hiyo, alimwuliza kilugha(alikuwa Muha): "unachukua au huchukui?"

Baada ya kumwuliza hivyo mara kadhaa, ndipo alimjibu kwa hasira, "sichukui". Alipojibu tu, babu yake alitoweka.

Alishangaa kwamba babu yake aliweza kumfuata mpaka huko wakati alikuwa anaamini kuwa ukishavuka maji, mchawi hawezi kumfuatilia tena. Yeye alivuka Ziwa Victoria lakini bado babu yake aliweza kumfuatilia.

Ni kweli hayo mambo hutokea katika ulimwengu wa kichawi?
 
kule ujerumani kuna chuo kikubwa sana cha uchawi kinaitwa Malheim Institute of Occult Practices,

sasa kule kuna kozi hiyo inaitwa teleportation and portal manipulation,

kimsingi huo uchawi ukiupata utaweza kusafiri juu ya maeneo ambayo field ya uchawi haifanyi kazi ie; kanisani, juu ya bahari...

hii ni kwasababu hautumii occult objects kama ungo na fagio, ila unatoweka na kutokea chini ya sekunde

ila ni uchawi mgumu sana kumaster

huyo mzee itakuwa ni alumnus wa huko au alipewa na alumnus wa huko
 
Mwambie amtafute Yesu kwa roho na kweli

Asiseme ati hauvuki maji Majini sio viumbe dhaifu Kama unavyofikiri speed yao ni kama umeme hawazuiwi na mlima,maji wala matter yoyote kwa sababu zile ni roho
Ndivyo nilivyoshauri, lakini siku chache baadaye kuna mambo yalinifanya nimtilie mashaka kama kweli yupo serious kiimani au la.
1. Alikuwa akijigamba kuwa hawezi kutapeliwa, na kwamba miaka ya nyuma kabla hajawa Mkristo, mtu aliyemtapeli hela ya kazi aliyomfanyia alimfuata mwenyewe baada ya kuondoka. Alidai alimpindisha mdomo.

2. Kuna siku kimbunga kilikuwa kinavuma kuelekea alikosimama. Alichofanya ni kunyoosha kidole na kukielekeza hicho kimbunga kielekee kuelekea mwingine. Na kweli kilibadili mwelekeo. Sijui kama nguvu aliyoitumia ilikuwa ni ya imani ya "Kweli", ushirikina au Saikolojia. Japo hakuwa ameniona, tokea siku hiyo, nilimtilia mashla kuwa huenda bado alikuwa na Imani ya kishirikina.

3. Alidai kuwa kabla ya kukataa kupokea mikoba ya kichawi, alikuwa ameshawahi kuona misukule, na alishawahi kushiriki kumwadhibu mtu mmoja kwa kumtoa ndani Usiku na kwenda kumlaza juu ya paa la nyumba. Mwathirika alijikuta Asubuhi yupo juu ya paa la nyumba yake ilahali mlango umefungwa kwa ndani.
 
Mbona inasemekana Wazungu hawajui uchawi?
 
ila zikija stori za dini una amini
kukataa stori za kichawi, na kukubali stori za dini lazima uwe mgonjwa

Nani kakwambia naamini hizo bedtime stories?

Wewe na ndevu zako unaamini mtu alitokea na kutoweka? Mtu kasimuliwa na yeye kaja kusimulia na wewe unaamini? Inabidi uwe zwazwa kiasi gani kuamini huu upupu?

Kwa akili zenu nikiwaambia namjua mtu aliyeenda sayari ya Pluto na kurudi mtaamini?
 
= kumrithisha.
 
Huo uliouhadithia siyo uchawi.
 
acha kujitia ujua ikiwa hujui chochote mkuu

uchawi upo na muumba yupo

alafu mnao pinga uchawi ndo wachawi wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…