GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kipindi fulani, nikiwa ninafanyia shughuli zangu maeneo ya machimbo ya dhahabu, nilifahamiana na kijana mmoja kutoka mkoani Kigoma. Alikuwa anafanya vibarua machimboni.
Kuna wakati alinifuata kwa ajili ya kuniomba ushauri. Aliniambia kuwa alikuja machimboni kama njia ya kumtoroka babu yake aliyekuwa akitaka kumridhisha uchawi. Japo kwa maelezo yake aliniambia kuwa alishawahi kushiriki kwenye matukio ya kichwawi, tena kipindi angali shule ya Msingi, kwa kipindi hicho alikuwa ameshaachana na hiyo tabia. Aliniambia alikuwa ameamua kuwa Mkristo. (Hata hivyo sikumwamini sana kama kweli alikuwa Mkristo kutokana na baadhi ya matukio aliyonisimulia na niliyoyashuhudia kwake).
Siku moja akiwa amelala kambini na wenzake, aliamka Usiku wa manane akaenda nje. Kitendo cha kutoka tu nje, alimkuta babu yake kajiinamia akiwa amejifunika vazi kama shuka au blanketi hivi.
Akiwa katika hali hiyo, alimwuliza kilugha(alikuwa Muha): "unachukua au huchukui?"
Baada ya kumwuliza hivyo mara kadhaa, ndipo alimjibu kwa hasira, "sichukui". Alipojibu tu, babu yake alitoweka.
Alishangaa kwamba babu yake aliweza kumfuata mpaka huko wakati alikuwa anaamini kuwa ukishavuka maji, mchawi hawezi kumfuatilia tena. Yeye alivuka Ziwa Victoria lakini bado babu yake aliweza kumfuatilia.
Ni kweli hayo mambo hutokea katika ulimwengu wa kichawi?