Ni kweli uchawi hauwezi "kuvuka" maji?

Ni kweli uchawi hauwezi "kuvuka" maji?

Labda sijakuelewa vizuri Mwl FaizaFoxy!

Unaweza ukanitofautishia uchawi na hiyo Elimu japo kwa maelezo mafupi?
Neno uchawi huwa na maana mbili.

Maana moja ni kuroga na kudhuru watu. Maana nyingine ni kufanya kitu ambacho wengine wengi hawakiwezi.

Uwezo wa kuwepo sehemu fulani mbali na kwenu, huo ni ujuzi tu.

Kuna watu wana uwezo wa kuonekana zaidi ya sehemu moja kwa wakati huo huo na hawana kabisa sifa ya uchawi. Sisi huita hizo ni karama (makarama).

Karama ni uwezo wa ujuzi au kipaji uliokirimiwa na Allah.

Karana zipo za aina nyingi sana na wanazo binadam.
 
Shikilia hapo hapo madam:
1. Kwa karne hii kuna watu wa aina hiyo?

2. Hao wanakuwa ni binadamu kamili au viumbe wanaofanana na binadamu lakini si binadamu?

3. Hapa Tanzania kuna watu wa aina hiyo?
 
Ni mpumbavu tu anaamini story yako. Story za kishirikia huwa ni hearsay stories za uongo uongo zisizo na chembe ya uthbitisho zinazoaminiwa na watu wajinga.
Unaishi nchi gani?

Unaposema watu wajinga, unamaanisha nini? Watu ambao hawajasoma?

Unajua kuna watu ambao pamoja na kuwa ni maprofesa, ni waumini wazuri wa uchawi, na wengine ni walimu wa uchawi?

Umeshasikia matukio yaliyoajiri Mwanza, Kigoma, Geita, n.k. ambako watu waliowahi kufa na kuzikwa walikuja kupatikana wakiwa hai? Polisi na viongozi wa Serikali waliotangaza hayo nao ni wajinga?
 
kule ujerumani kuna chuo kikubwa sana cha uchawi kinaitwa Malheim Institute of Occult Practices,

sasa kule kuna kozi hiyo inaitwa teleportation and portal manipulation,

kimsingi huo uchawi ukiupata utaweza kusafiri juu ya maeneo ambayo field ya uchawi haifanyi kazi ie; kanisani, juu ya bahari...

hii ni kwasababu hautumii occult objects kama ungo na fagio, ila unatoweka na kutokea chini ya sekunde

ila ni uchawi mgumu sana kumaster

huyo mzee itakuwa ni alumnus wa huko au alipewa na alumnus wa huko
Ulifanikiwa kupata certificate?
 
Mimi nipo Gronelberg University of Sorcery and Mysticism, napiga shahada ya Shapeshifting.

Nikimaliza naenda pale Magnum Valsen Canada kupiga shahada ya Assault magic.
Ajira yake inakuwaje;
Au unafungua kanisa la upako, au utapeli, au uganga wa kienyeji, Au utajiri wa kimiujiza?

Vipi upo chuo kimoja na Harry Potter au fiction story. Gamboshi wanatoa level gani ya elimu. Je ni kweli kuna dark witch na white witch.

Samahani kwa maswali yasiyopangiliwa. Just curious
 
Unaishi nchi gani?

Unaposema watu wajinga, unahamisha nini? Watu ambao hawajasoma?

Unajua kuna watu ambao pamoja na kuwa ni maprofesa, ni waumini wazuri wa uchawi, na wengine ni walimu wa uchawi?

Umeshasikia matukio yaliyoajiri Mwanza, Kigoma, Geita, n.k. ambako watu waliowahi kufa na kuzikwa walikuja kupatikana wakiwa hai? Polisi na viongozi wa Serikali waliotangaza hayo nao ni wajinga?

Toa mfano wa mtu mmoja tu aliyethibitika kufariki na kufufuka? Zingatia neo "aliyethibitika" sio story za wajinga za hearsay.

Nyie watu mkiambiwa chochote tu mnaamini kama nyumbu.

Zwazwa mwingine alileta story kama yako hapa JF 2021 eti diwani alikufa na kutokea huko huko Kigoma. Mind you diwani ni ofisi ya umma majina na makazi yake ni public record. Nilimuuliza swali moja tu, taja jina la hiyo diwani. Hadi leo hajataja ila watu wajinga wajinga waliamini ile story. Niliahidi kutoa laki 5 TSH kwa mtu yeyote atayenipa jina la huyo diwani, so kama wewe unamfahamu huyo diwani naomba jina lake tu nitakupa laki 5 TSH. Hadi leo toka 2021 sijaepewa jina tu. Uzi huu hapa chini:

Ajira yake inakuwaje;
Au unafungua kanisa la upako, au utapeli, au uganga wa kienyeji, Au utajiri wa kimiujiza?

Vipi upo chuo kimoja na Harry Potter au fiction story. Gamboshi wanatoa level gani ya elimu. Je ni kweli kuna dark witch na white witch.

Samahani kwa maswali yasiyopangiliwa. Just curious
1. Ajira, unajiunga na legion. Legion ni taasisi za kichawi zenye mielekeo mbalimbali, lengo kuu likiwa ni kuwaondoa wanadamu kwenye utukufu wa Mungu.

Mfano mimi nikiwa na shahada ya shapeshifting, naweza kuajiriwa kwenye Legion of malistic interventions, hapo kazi inakuwa ni kuingilia matukio muhimu kwenye maisha ya watu kama kupata kazi, kuoa nk

2. Uganga wa kienyeji, ni freelancing, hao ni wachawi waliorithishwa nguvu, hawajajifunza kutoka mwanzo, ni second handlers.
Raha ya kujifunza ukawa first handler kwenye hivi vyuo, ni kwamba ajira zake zina manufaa sana(hata ya kimali) kuliko freelancing.

3. Hogwarts ya harry potter ni fictional story, aliyeandika amesikia hayo mambo kichini chini tu

4. Kimsingi hakuna, ukijaribu kutumia uchawi kwa lengo linalolandana na hoja no.1 unakuwa powerless.
Lakini migogoro ya utekelezaji kazi inatokea sana baina ya wachawi.

5. Gambosh ni kama hogwarts tu, stori za vijiweni.
 
Kipindi fulani, nikiwa ninafanyia shughuli zangu maeneo ya machimbo ya dhahabu, nilifahamiana na kijana mmoja kutoka mkoani Kigoma. Alikuwa anafanya vibarua machimboni.

Kuna wakati alinifuata kwa ajili ya kuniomba ushauri. Aliniambia kuwa alikuja machimboni kama njia ya kumtoroka babu yake aliyekuwa akitaka kumridhisha uchawi. Japo kwa maelezo yake aliniambia kuwa alishawahi kushiriki kwenye matukio ya kichwawi, tena kipindi angali shule ya Msingi, kwa kipindi hicho alikuwa ameshaachana na hiyo tabia. Aliniambia alikuwa ameamua kuwa Mkristo. (Hata hivyo sikumwamini sana kama kweli alikuwa Mkristo kutokana na baadhi ya matukio aliyonisimulia na niliyoyashuhudia kwake).

Siku moja akiwa amelala kambini na wenzake, aliamka Usiku wa manane akaenda nje. Kitendo cha kutoka tu nje, alimkuta babu yake kajiinamia akiwa amejifunika vazi kama shuka au blanketi hivi.

Akiwa katika hali hiyo, alimwuliza kilugha(alikuwa Muha): "unachukua au huchukui?"

Baada ya kumwuliza hivyo mara kadhaa, ndipo alimjibu kwa hasira, "sichukui". Alipojibu tu, babu yake alitoweka.

Alishangaa kwamba babu yake aliweza kumfuata mpaka huko wakati alikuwa anaamini kuwa ukishavuka maji, mchawi hawezi kumfuatilia tena. Yeye alivuka Ziwa Victoria lakini bado babu yake aliweza kumfuatilia.

Ni kweli hayo mambo hutokea katika ulimwengu wa kichawi?
itabidi sasa na mm niweke swiming pool mbele ya mlango wangu huu.
 
Neno uchawi huwa na maana mbili.

Maana moja ni kuroga na kudhuru watu. Maana nyingine ni kufanya kitu ambacho wengine wengi hawakiwezi.

Uwezo wa kuwepo sehemu fulani mbali na kwenu, huo ni ujuzi tu.

Kuna watu wana uwezo wa kuonekana zaidi ya sehemu moja kwa wakati huo huo na hawana kabisa sifa ya uchawi. Sisi huita hizo ni karama (makarama).

Karama ni uwezo wa ujuzi au kipaji uliokirimiwa na Allah.

Karana zipo za aina nyingi sana na wanazo binadam.
Waulize kuna watu nasikia wanaufuata mpaka pemba. Mbona unavuka bahari bila shida. Huko mtaani watu wanwaogopa wapemba kuwa wachawi sana na kuogopa hata kuwaibia au dhuluma. Labda kuna Ukweli. Je huo uchawi mbona umevuka bahari?
 
Shikilia hapo hapo madam:
1. Kwa karne hii kuna watu wa aina hiyo?

2. Hao wanakuwa ni binadamu kamili au viumbe wanaofanana na binadamu lakini si binadamu?

3. Hapa Tanzania kuna watu wa aina hiyo?
Naam, wapo kijana. Kuna watu wamejaaliwa vipawa aina mbali mbali. Utaona ajabu. Tanzania wapo, lakini huwezi kuwajuwa mpaka ushuhudie au uhadithiwe na watu unaowaamini.

Binafsi nilibahatika kufahamiana na watu wawili Tanzania ambao nilikuwa nashangaa elimu yao wanaipata wapi. Hao watu mmoja ni mwanafunzi wa mwingine. Huyo Mwalim au niseme Maalim, ni mmoja katika Walimu wa marehemu mzee Ali hassan mwinyi. Alikuwa ni Mzanzibari mwenye asili ya visiwa vya ngazija. (Comoro).

Wazanzibari, watu wa Bara, Wacomoro, Wakenya na wasomi wengi wa Kimataifa wakimfaham sana. Nilibahatika kumfaham yeye na mwanafunzi wake, ambae kwa sasa pia ni Marehemu.

Maaruf, Mwinyi baraka , Sheikh Omar bin Abdallah.

Ukikutana na wanafunzi wake au wanafunzi wa wanafunzi wake utastarehe wakikuhadithia mambo yake. Mengine ni utaona ni miujiza, lakini ni elimu tu.
 
Back
Top Bottom