Ni kweli Vatican wanakataa kumpa Uaskofu Padri Kitima baada ya kupata tetesi anataka kugombea ubunge kupitia CHADEMA?

Jimbo gani?
 
Kwa kweli mada imekuja km swali, mimi binafsi kwa kweli sijui kwa hiyo sina jibu lake! 😄
 
Unahisi uaskofu ni haki yake kwamba anaupata kwa matakwa.
Unataka kutuaminisha kuwa ndani ya kanisa katolic Tanzania Padri Charles Kitima anaweza akaamua lolote?
 
Askofu Mkuu wa Jimbo katoliki la Bukoba ni muhashamu Baba askofu Jovitus Francis Mwijage

Huyo Methodius Kilaini ni askofu kamili wa jimbo gani gani?
Kwa hiyo hoja yako Askofu Kilaini siyo askofu
 
Kwani kilaini sio askofu?
Ni Askofu msaidizi tu, full stop.
Ana barua ya Baba Mtakatifu ya kua askofu msaidizi tu.

Nzigilwa na Eusebius wana barua za kuteuliwa kuwa maaskofu wa saidizi dar, lakini pia wana barua za kuteuliwa maaskofu wa majimbo.

Mama hawezi kua Baba and vise versa is true, lakini wote ni wanandoa.
 
Jibu sahihi ni kwamba anataka kugombea ubunge kupitia CCM.
Asingekuwa anashinda machame, mpaka Mzee mbowe kaagiza apewe chumba chake maalum
 
Baba Askofu wa Jimbo Katoliki lolote duniani mara anapokalia kiti cha Kiaskofu mojawapo ya majukumu yake ya mwanzo ni kupendekeza majina matatu ya Mababa Mapdre ya kuwa kutoka Jimbo lake wanaweza kuteuliwa kuwa Mababa Askofu kutokana na vigezo vilivyowekwa. Kaa nayo kichwani hiyo.
 
Maaskofu wa Roman hawapigiwi kura,kujisimika au kujitunuku uaskofu kama wengine wanaojipachika utume na unabii baada ya kukariri vifungu kwenye biblia.
Mchakato ni mrefu na unachukua miaka mingi,hata mlengwa anakuwa haijui kinachoendelea bali anakuwa taken by surprise.
 
Hayo ni majina ya kupendekeza warithi wake, lakini siyo lazima watoke kwenye hayo majina. Askofu mstaafu wa Lindi kwenye interview Moja alisema hakudhani kama huyu askofu wa Sasa WA lindi (Wolfgang) ndiye atakuwa mrithi wake, alikuwa anawawazia wengine kabisa
 
Yaani umelishwa matango pori na huo jamaa yako huko uliko, halafu unakuja kuyatapikia kama yalivyo humu jukwaani!! This is not fair at all.
Hakuna mtu yeyote aliyemwambia. Hizo ni chuki binafsi alizo nazo kwa Kitima. Kitima hapo alipo ni zaidi ya mbunge atambue hilo. Wasiwakatae watu wanaowashauri.
 
Kweli na ukifuatilia utàkuta alipendekzwa na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki jengine ila akapelekwa huko.
 
Mtoa hoja hujui chochote kuhusu ukatoliki. Katibu Mkuu wa TEC ni mtu mkubwa saaaaana kuliko Askofu. Majukumu yake ni makubwa. Hawezi kuwa Askofu. Huyo ndio Boss wao. Ndio maana ili uwe Katibu wa TEC lazima uwe na elimu ya kitosha sana. Kwa itofaki yeye ndiye anayeongoza utendaji wa Baraza la Maaskofu, lenye nguvu zaidi Tanzania.
 
Kwa kawaida utaratibu wa kanisa katoliki haliruhusu mapadri kugombea ngazi yoyote ile ya kisiasa labda kama utajivua gamba kama alivyofanya dr slaa au Dr mhagama mbunge wa madaba.Ni kweli padri kitima ni mwimini wa cdm ukimwondoa nje ya ukasisi wake kama binadamu.na mchakato wa kujitoa kwenye upadre uko so complicated na hii ndo hali halisi.
 
Kila anachokiongea Fr. Kitima kina baraka za kanisa na ndio maana mpaka sasa bado ni katibu mkuu wa TEC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…