Labda ungerejea argument imeanzia wapi. Ni je! Kilaini ni askofu kamili au la! Jibu ni: Kilaini ni askofu kamili.
Rejea swali lako ulipouliza: 'Kilaini ni askofu kamili wa jimbo gani?'
Jibu ni: Askofu sio lazima awe na jimbo ndio awe askofu kamili. Unaweza kuwa askofu lakini ukapewa majukumu mengine, tofauti na jimbo, kwa mfano 1) Kardinali Protase Rugambwa (hapo awali) alikuwa askofu wa jimbo la Kigoma. Baadae akatolewa, akapelekwa Rome kuwa katibu wa idara ya uenezaji injili- bado ni askofu kamili. 2) Askofu mkuu Novatus Rugambwa hajawahi kuwa na jimbo, anafanya kazi za kidipolmasia- (balozi wa Vatican sehemu mbalimbali)- bado ni askofu kamili. 3) Maaskofu Kilaini, Mchamungu,/Stephano Musomba na Prosper Lyimo, ambao ni maaskofu wasaidizi, hawa wote ni maaskofu kamili.