Huyu Dada Wastara kweli alipata maswahibu, na jamii ya Tanzania iliguswa sana. Binafsi sijawah kumchangia na wala sina kawaida ya kuchangia mastaa, sadaka yangu hua naitoa kwa wahitaji waliosetwa na hua ninasaidia kwa siri kubwa kiasi kwamba mkono wa kuume unapotoa basi mkono mwingine usijue kabisa kinachoendelea kama yanavyoagiza maandiko.
Huyu Wastara sasa kachangiwa na kiongozi wa nchi akapate matibabu ughaibuni. Kitendo cha yeye kuleta maigizo (kama ni kweli) ili atafune pesa ni jambo baya na linaaibisha haiba ya waliomchangia. Anawadhihirishia kwamba yeye ni mjanja sana na wao ni mabwegwe, yumkini! Hili litamcost sana, ikithibitika. Lazima mamlaka itamfanyia ushushushu akirudi au yumkini "watu" wapo nae huko aliko bila yeye kujua.
Namuombea sana isiwe kweli.