Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Leo mheshimiwa Lissu amelihutubia Taifa na kulieleza hatua kwa hatua juu ya uamuzi wa chama cha CHADEMA kuwa KAMA HAKUNA MABADILIKO YA MSINGI KWENYE KATIBA NA SHERIA zinahosu uchaguzi nchini basi CHAMA hicho HAKITAKUBALI Uchaguzi feki ufanyike nchini mwezi october 2025.
Akiongea kwa nukta, huku akieleza kwa takwimu na mifano halisi, Lissu amewafumbua macho watanzania kuwa PROCESS nzima ya Tanzania inayohusika na uchaguzi haiwezi kutoa uchaguzi huru na haki, na ushahidi wa hilo ni chaguzi nyingi zilizopita toka mwaka 1995.
Lissu akaeleza kuwa kwa sasa nchini HAIWEZEKANI kamwe kukawa na uchaguzi wo haki, maana CCM imeondokewa na haya kabisa.
Ndugu Lissu akaainisha matatizo kuanzia.
1)Daftari la Mpiga kura ambalo utaratibu wa kuliupdate na kupata taarifa zake inakuwa ni tabu.
2)Magumashi kipindi cha ratiba za kampeni na uhuni mwingi kwa mfano kipindi cha kampeni vyombo vya habari vya umma huwa vinageuka Mouthpiece ya CCM. Havina fairness yoyote.
3) Akazungumza kuhusu magumashi kwenye kuwaengua wagombea wa upinzani.
4) Akazungumzia magumashi kwenye kuwaengua mawakala wa kusimamia uchaguzi wa vyama vya upinzani.
5) Akazungumzia magumashi kwenye kupiga kura
kama vile maboksi ya kura kuchukukuliwa na mapolisi chini ya mtutu wa bunduki na ukisimama ktk njia yao wanakupiga risasi.
6)Akazungumza kuhusu kura feki ambazo CCM wanajiongezea, mfano mwaka 2020 kuna zaidi ya kura milioni 2, ziliongezeka kinyume na idadi ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura.
7)Akazungumza juu ya wateule wa NEC na wasimamizi wa uchaguzi ambao kimsingi ni watu wa rais ambaye ni mgombea pia.
Lissu akahoji wanaCHADEMA wenye kutaka kugombea, kuwa unawezaje kugombea ktk mazingira kama haya wakati unajua unapeleka kichwa chako ili uchinjwe?.
Lissu akawataka viongozi wa dini na taasisi nyingine nchini ziiunge mkono CHADEMA kwenye azma yake ya kuhakikisha sasa ndiyo mwanzo na mwisho wa chaguzi feki nchini. Akasema hii ni nchi yao pia wana wajibu wa kuhakikisha haki inatamalaki nchini.
Kisha akasema kuwa NO REFORMS NO ELECTION ( Bila mabadiliko ya msingi nchini, basi uchaguzi haufanyiki) ni UAMUZI wa kikao cha juu kabisa cha chama yaani mkutano mkuu cha tarehe 21/1/2025. Kwa hiyo siyo maamuzi yake binafsi yeye kama yeye.
MY TAKE:
Lissu sasa ametuonyesha njia njema, tumemuelewa na tunamuunga mkono. Kwa kweli kuingia kwenye chaguzi huku ukijua unaenda kushiriki uchafuzi ni ujinga, ni kupoteza muda, ni kupoteza hela, kodi za wananchi. Sisi tunaunga mkono wa kupata KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI.
Soma Pia:

