Pre GE2025 Tundu Lissu afafanua No Reform No Election, hatuzungumzii kususia uchaguzi na hatutasusia bali Uchaguzi hautofanyika!

Pre GE2025 Tundu Lissu afafanua No Reform No Election, hatuzungumzii kususia uchaguzi na hatutasusia bali Uchaguzi hautofanyika!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wenye macho tumeshaona kuwa, yatafanyika mabadiliko kikatiba kwenye Sheria ya Uchaguzi, na tutapiga kura Kwa HAKI.

Hilo halitakuja kwenye sahani kama hisani, Bali ni Kwa shinikizo Toka ndani na nje.

Karibu sana Donald Trump!

Na ubarikiwe TUNDU Lissu.

Ubarikiwe Simba Judge Warioba!

Amen
 
Hii kauli ya risu imeshaanza kuleta impact uandikishaji wa wapiga kura umeanza kusuasua
 
No reforms, no elections, ni nzuri, kama wana hiyo popular support, na kama watafanya mambo hayo kwa amani, wamesema watafanya civil disobedience kwa amani, na watazungumza na wafadhili.

Kama wafadhili wata respond, wanatakiwa warespond, kwa namna ambayo haitaumiza wananchi (may be in a peaceful and targeted way).

Lissu yuko sahihi pia kusema kwamba mbunge wa viti maalumu aliekaa bungeni muda mrefu, akagombee jimboni, endapo chadema itashiriki uchaguzi.

Lissu na wafuasi wake ndani ya chadema, wawe free kabisa kuiongoza chadema.

Wabunge 19 wanawake wa chadema, au wabunge wowote wa zamani wa chadema, wanaweza waka angalia upepo unavyoenda, kama wanaona hawana future nzuri ndani ya chadema, wanaweza wakaongea na wapiga kura wao majimboni, kuona kama wagombee kwa tiketi ya ccm.

Nadhani Mbowe aongee na wapiga kura wa jimbo la Hai, kama wanataka agombee ubunge au asigombee ubunge.

Na kama agombee, je ni kupitia chadema au ccm. Kama kupitia chadema ok. Kama kupitia ccm, basi ajiunge na ccm. Na akishinda ubunge, na ccm ikishinda uchaguzi, saa100 anaweza kumteua Mbowe kuwa waziri mkuu wa Tanzania.

Wengine wanaoweza kuwa waziri mkuu wa Tanzania ni Mkenda, Mwigulu, Kabudi, au mbunge mmoja atakae toka eneo la usukumani (kabila lake awe ni msukuma, na sio mtu wa mkoa wa Mara).

Waprotestanti wapewe preference kwenye nafasi ya uwaziri mkuu, kama hakuna mprotestanti anaefaa, basi waziri mkuu awe mkatoliki (kama Mkenda). Waziri mkuu atoke mbali na kusini, as Nchimbi makamu wa rais mtarajiwa anatokea kusini tayari.

Majaliwa anaweza kuendelea kuwa waziri, na sio waziri mkuu. Kimei anaweza kuteuliwa kuwa naibu waziri wa wizara fulani.

Mtu yeyote wa chadema ambaye, anaona kwamba hata fikia potential yake chini ya uongozi mpya wa chadema, anaweza akawa mpole au anaweza akahamia ccm. Ccm isiwatumie watu wanao hamia kutoka chadema, kama nyenzo ya propaganda mbaya, dhidi ya wenzao waliobaki huko chadema.

Vuguvugu la uzalendo limeongezeka, hususan baada ya Tundu Lissu kushinda chadema. Inaelekea kanisa katoliki limeongeza uwekezaji wao huko chadema. Naona pia mkoa wa Mara umeongeza uwekezaji wao huko chadema.

Inabidi Saa100, kama anaweza, a renegotiate mikataba yote mibovu na aifanye iwe na maslahi na ustawi mzuri kwa watanzania.

Abalance vizuri uzalendo, haki za binadamu na demokrasia, huku akiendelea kuwa na mahusiano mazuri na mataifa yenye nguvu duniani. Awe pia na mahusiano mazuri na mikoa yote ya Tanzania. Awe pia na mahusiano mazuri na wachagga.

Saa100 pamoja na bunge, wanaweza wakapitisha sheria ya kuruhusu urais kuwa term tatu, za miaka mitano kila term. Au urais kuwa term mbili, za miaka sita kila term. Wabunge na madiwani wawe na terms za miaka sita, na sio mitano kama ilivyo sasa.

Kwa sasa hii inawezekana, as karibia bunge lote ni ccm. Term za miaka 6, zitapunguza gharama za uchaguzi mkuu.

Miaka saba hapana, ni mingi sana.

TZ diaspora walio acha uraia wa Tanzania, wapewe muhuri wa permanent resident (au permanent leave to remain), kwa urahisi sana, kwenye passport zao mpya za kigeni. Wanaweza pia wakapewa special status, ambayo pia ita include hayo hapo juu.

Umri wa kukana au kuchagua uraia kwa watoto wa kiTZ wenye fursa ya uraia wa zaidi ya nchi moja, uwe ni miaka 30, na sio miaka 18 kama sasa.

Hii itawawezesha watoto hao wa kiTZ kunufaika na elimu nzuri na ya gharama nafuu hadi chuo kikuu, huko ughaibuni.

Umri wa chini wa kuruhusiwa kufanya vitu ambavyo sio vizuri, upandishwe kutoka miaka 18 hadi miaka 21, kama matumizi ya pombe/alcohol, sigara/tobacco/shisha, kamari/sportsbetting/casino/lottery, kwenda disco/nightclub, cinema za miaka 18 huko nje, hapa ziwe ni miaka 21.

Pia shisha au na aina zote za kamari, ziwe regulated au banned, kama vimekuwa out of control.

Umri wa kupiga kura ushushwe na uwe ni miaka 15. Umri wa kufanya kazi nyepesi uwe ni miaka 15. Umri wa kufanya kazi nzito uwe ni miaka 21.

Umri wa kuruhusiwa kujiunga na majeshi uwe ni miaka 21; wakati wa vita, umri huo unaweza kushuka na kuwa miaka 18.

Umri wa kuoa au kuolewa, na wa kuruhusiwa kufanya mapenzi uwe ni miaka 21. Watu wenye umri wa miaka 18, wataweza kuoa au kuolewa kwa ridhaa ya wazazi.

Umri wa kuendesha gari uwe ni miaka 18 (class B na D). Umri wa kuendesha magari makubwchademai miaka 21.

Saa100, inabidi aendelee na concept ya TZ as a developmental state.
 
Kila taifa lina taratibu zake za kiuchaguzi duniani, kwa tanzania taratibu safi tulizojiwekea ndizo tunazozifuata!
Za kuiba kura? Za kuteka na kuuwa wapinzani wako? Taratibu za wakurugenzi kufunga ofisi ili mpinzani akirudisha fomu asikukute ofisini? Taratibu za kuzuia vyombo vyote vya habari visiipe air time CHADEMA.
 
Za kuiba kura? Za kuteka na kuuwa wapinzani wako? Taratibu za wakurugenzi kufunga ofisi ili mpinzani akirudisha fomu asikukute ofisini? Taratibu za kuzuia vyombo vyote vya habari visiipe air time CHADEMA.
Tuseme, hamad, chadema imeshinda, je unafikiri haita ifanyia CCM, figisu? Off-course haliwezekani kutokea, acha ccm wakaze butt!
 

Leo mheshimiwa Lissu amelihutubia Taifa na kulieleza hatua kwa hatua juu ya uamuzi wa chama cha CHADEMA kuwa KAMA HAKUNA MABADILIKO YA MSINGI KWENYE KATIBA NA SHERIA zinahosu uchaguzi nchini basi CHAMA hicho HAKITAKUBALI Uchaguzi feki ufanyike nchini mwezi october 2025.

Akiongea kwa nukta, huku akieleza kwa takwimu na mifano halisi, Lissu amewafumbua macho watanzania kuwa PROCESS nzima ya Tanzania inayohusika na uchaguzi haiwezi kutoa uchaguzi huru na haki, na ushahidi wa hilo ni chaguzi nyingi zilizopita toka mwaka 1995.

Lissu akaeleza kuwa kwa sasa nchini HAIWEZEKANI kamwe kukawa na uchaguzi wo haki, maana CCM imeondokewa na haya kabisa.

Ndugu Lissu akaainisha matatizo kuanzia.

1)Daftari la Mpiga kura ambalo utaratibu wa kuliupdate na kupata taarifa zake inakuwa ni tabu.

2)Magumashi kipindi cha ratiba za kampeni na uhuni mwingi kwa mfano kipindi cha kampeni vyombo vya habari vya umma huwa vinageuka Mouthpiece ya CCM. Havina fairness yoyote.

3) Akazungumza kuhusu magumashi kwenye kuwaengua wagombea wa upinzani.

4) Akazungumzia magumashi kwenye kuwaengua mawakala wa kusimamia uchaguzi wa vyama vya upinzani.

5) Akazungumzia magumashi kwenye kupiga kura
kama vile maboksi ya kura kuchukukuliwa na mapolisi chini ya mtutu wa bunduki na ukisimama ktk njia yao wanakupiga risasi.

6)Akazungumza kuhusu kura feki ambazo CCM wanajiongezea, mfano mwaka 2020 kuna zaidi ya kura milioni 2, ziliongezeka kinyume na idadi ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura.

7)Akazungumza juu ya wateule wa NEC na wasimamizi wa uchaguzi ambao kimsingi ni watu wa rais ambaye ni mgombea pia.

Lissu akahoji wanaCHADEMA wenye kutaka kugombea, kuwa unawezaje kugombea ktk mazingira kama haya wakati unajua unapeleka kichwa chako ili uchinjwe?.

Lissu akawataka viongozi wa dini na taasisi nyingine nchini ziiunge mkono CHADEMA kwenye azma yake ya kuhakikisha sasa ndiyo mwanzo na mwisho wa chaguzi feki nchini. Akasema hii ni nchi yao pia wana wajibu wa kuhakikisha haki inatamalaki nchini.

Kisha akasema kuwa NO REFORMS NO ELECTION ( Bila mabadiliko ya msingi nchini, basi uchaguzi haufanyiki) ni UAMUZI wa kikao cha juu kabisa cha chama yaani mkutano mkuu cha tarehe 21/1/2025. Kwa hiyo siyo maamuzi yake binafsi yeye kama yeye.

MY TAKE:
Lissu sasa ametuonyesha njia njema, tumemuelewa na tunamuunga mkono. Kwa kweli kuingia kwenye chaguzi huku ukijua unaenda kushiriki uchafuzi ni ujinga, ni kupoteza muda, ni kupoteza hela, kodi za wananchi. Sisi tunaunga mkono wa kupata KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI.

Soma Pia:
Tuelewe kwamba utukutu mwingine hauna maana. Hata kama CHADEMA hawakubaliani na mfumo uliopo, kundi la watu wachache haliwezi kuingilia haki ya watu walio wengi kuchagua viongozi wao. Nafikiri wanaweza kuchukuliwa hatua kama watajaribu kutekeleza wanacho kipanga
 
Tuseme, hamad, chadema imeshinda, je unafikiri haita ifanyia CCM, figisu? Off-course haliwezekani kutokea, acha ccm wakaze butt!
Kuna mambo mawili CHADEMA wanaweza kusamehe na kusahau unyama wote waliofanyiwa na ccm kwa miaka 30; Au wakaamua kulipa kisasi yote waliyofanyiwa na ccm kama kuuwawa kutekwa kuvunjiwa nyumba na kuharibiwa biashara kuzuiwa mikutano yao NK. Either of the way watakayoichagua CHADEMA itakuwa sahihi.
 
Tuelewe kwamba utukutu mwingine hauna maana. Hata kama CHADEMA hawakubaliani na mfumo uliopo, kundi la watu wachache haliwezi kuingilia haki ya watu walio wengi kuchagua viongozi wao. Nafikiri wanaweza kuchukuliwa hatua kama watajaribu kutekeleza wanacho kipanga
Kwa upumbavu wenu mnadhani chadema wanafanya haya kwa faida yao hapana CHADEMA wanafanya haya kwaajili ya kuokoa vizazi vyenu.
 
Tuelewe kwamba utukutu mwingine hauna maana. Hata kama CHADEMA hawakubaliani na mfumo uliopo, kundi la watu wachache haliwezi kuingilia haki ya watu walio wengi kuchagua viongozi wao. Nafikiri wanaweza kuchukuliwa hatua kama watajaribu kutekeleza wanacho kipanga

Bongo hakuna haki ya kupiga kura, ingekuwepo ingeweza kudaiwa mahakamani
 
Hoja za CHADEMA kuhusu uchaguzi zipo very clear.

CCM/Serikali kushindwa kujibu hoja hizo ni kuwatangazia Watanzania na Dunia kwamba madai ya CHADEMA ni sahihi na ni sahihi kweli kweli.
 
Sio ni lini CCM sema ni lini serikali itatajibu hoja za CHADEMA
 
Back
Top Bottom