Majibu ya Kisheria kwa Ndugu Tanganyikani: Heche Atajiuzulu kwa Prima Facie Ipi au Ni Njaa za Kijiweni Zinawasumbua?
Ndugu Tanganyikani na genge lako la
"Makamanda wa mchongo" mnaoshinda mitandaoni mkitetemeka kama kuku walionyeshewa na mvua kwa kila uzushi mnaousoma; salama sana.
Nimesoma kwa masikitiko makubwa bandiko lako linalohoji ni lini Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara),
Mheshimiwa John Heche, atajiuzulu kupisha uchunguzi wa kimahakama ya kahawa mliyofungua huko Handeni. Ili kukuponya na ugonjwa huu wa upofu wa kisheria na kisiasa, naomba nikushushie dozi hii ya hoja kavukavu ili ukawafunge midomo hao mabwana zako mnaoshinda nao vijiweni:
1. Persona Non Grata Kisheria: Ofisi ya Heche na Suala la Fedha
Kisheria na Kikatiba, unapoanzisha madai ya mtu kujiuzulu, lazima uonyeshe
prima facie (ushahidi wa awali wa msingi) unaomunganisha mtuhumiwa na kosa husika. Katika mfumo wa kisheria wa CHADEMA, Makamu Mwenyekiti hana mamlaka yoyote ya kiutendaji ya kifedha (
not an Accounting Officer). Msimamizi mkuu wa mapato, matumizi, na mali zote za chama kisheria ni
Katibu Mkuu, Mhe. John Mnyika.
Kumtaka Heche ajiuzulu kwa madai ya ubadhilifu wa fedha za Handeni ni sawa na kwenda mahakamani kumshtaki Waziri wa Mambo ya Nje kwa makosa ya ukusanyaji kodi wa TRA. Huku ni kukosa uelewa wa kimsingi wa sheria (
sheer legal ignorance) na kujivua nguo hadharani.
2. Udhaifu wa Ushahidi na Kanuni ya Hear-Say (Maneno ya Kusikia)
Popote duniani, kiongozi hawezi kuwajibika kwa sababu tu ya "waraka wa mtu mwenye njaa" au "video ya clip ya sekunde 30" iliyorekodiwa kwenye korido za baa. Madai yenu yote yanaangukia kwenye kundi la
hearsay evidence (ushahidi wa kusikia)—ambao hauna mashiko mbele ya vikao halali vya chama wala mahakama yoyote huru.
Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Tanga ulishatoa tamko rasmi na kuuzika huo uzushi, ukifafanua kuwa kile kilikuwa ni kikundi cha mamluki waliotengeneza sarakasi ili kukwamisha harakati za chama. Kama ripoti rasmi ya ukaguzi wa ndani (
Internal Audit Report) haijamtia hatiani Heche, kelele zenu za mitandaoni ni sawa na mbwa anayeuzunguka mti akibwekea ndege aliyeko angani.
3. Agenda ya Kupikwa Kuhama Kwenye Reli
Mh. John Heche hivi sasa yuko busy mikoani akisimamia Operesheni za Katiba Mpya na kupigania haki za viongozi wenu wanaosumbuliwa na kesi za kusingiziwa. Huu mtego wenu wa kitoto wa kutaka ajiuzulu umelenga kumtoa kwenye reli ili kuhamisha mjadala wa kitaifa. Hamuwezi kutupangia agenda kwa kutumia matamko ya kununuliwa kwa bei ya doti ya khanga.
NB: Ndugu Tanganyikani, hebu tuvue vinyago hapa. Inaonekana dhahiri wewe si mwanachama wa CHADEMA kama unavyojinasibu kwa unafiki hapa jukwaani. Wewe ni miongoni mwa wale
"Machawa" wa kijani (CCM) msio na aibu, mnaojivika ngozi ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu. Unajiziba kwenye mgongo wa kashfa za uongo za kutengeneza mitandaoni ili kumchafua Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa John Heche. Kamanda gani goli la kwanza tu la propaganda za kijinga unakuwa wa kwanza kulia na kuweweseka mitaani? Nenda kachukue posho yako hapo lumumba, huku CHADEMA hakuna nafasi ya wapika majungu!
OUR MOTTO: THE WHOLE PLAN IS A NEW CONSTITUTION AND ELECTORAL REFORM! ✊🔥