Ni lini mapendekezo ya Ripoti hizi yatafanyiwa kazi?

Ni lini mapendekezo ya Ripoti hizi yatafanyiwa kazi?

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,730
Reaction score
2,230
Danadana zinaendelea na kuendelea kutafuna fedha za umma. Ya Nyalali yalitupwa, Kisanga alifokewa na Mkapa, Warioba akashambuliwa na Kikwete na hadi kupigwa ngwala na kijana wake Makonda ambaye alipewa zawadi ya ukuu wa wilaya ya Kinondoni.

Na huyu kaja na "si amri" - danadana zinaendelea!

Nyalali: Season 1
Kisanga: Season 2
Warioba: Season 3
Mukandala: Season 4
Nanihii (!?): Season 5
...tunasuburi
 
Huwezi kukata Tawi ulilolalia
Kama Erythrocyte et al wangekuelewa, wangalijua kuwa JPM alikuwa mzalendo wa nchi hii maana hakulemba au kupindisha maneno.

Upuuzi wa kumaliza hela zinazotakiwa kuleta maendeleo! Nani ajitie kitanzi? Nani aingize kichwa chake katika mdomo wa mamba?

Samia apunguze madaraka yake kweli? Huyo atakuwa ni binadamu au fisi? Tume huru ili asiibe kura kweli na asaini hiyo kitu!!!!

Ati matokeo yapingwe mahakamani akina Tindo wanashangilia wakati huo huo Samia anasema atagombea 2025! Hivi akili gani hizi Vijana wa chadema!!!!!!!! Mystery unaamini?

Uliona jinsi ambavyo Rais wa USSR alivyokubali kujitia kitanzi aliishia hata kutozikwa na Putin. Unadhani Kikwete atakubali kesho aipate kama JPM alivyomsulubu! Mnatania nyie watu.

Mbona hakuna anayezungumzia mgombea binafsi maana akina Zitto, Tundu Lissu na akina MBOWE wanajua hicho ni Kifo chao, Asali inayoyoma wakikubali mgombea binafsi!
 
Danadana zinaendelea na kuendelea kutafuna fedha za umma. Ya Nyalali yalitupwa, Kisanga alifokewa na Mkapa, Warioba akashambuliwa na Kikwete na hadi kupigwa ngwala na kijana wake Makonda ambaye alipewa zawadi ya ukuu wa wilaya ya Kinondoni.

Na huyu kaja na "si amri" - danadana zinaendelea!

Nyalali: Season 1
Kisanga: Season 2
Warioba: Season 3
Mukandala: Season 4
Nanihii (!?): Season 5
...tunasuburi
Danadana !! Ukipiga danadana kwa muda mrefu ni lazima utakosea na mpira utadondoka chini !! Waulize wacheza mpira wa miguu kama nasema uongo !!
 
Mkuu kolola , naunga mkono hoja.
P
Mheshimiwa, hawa Watoto ni Bendera fuata Mkumbo! Mchakato wa katiba au mabadiliko hutokana na msukumo wa jamii! Mabadiliko hayaletwi kwa sahani. Jinsi ya kupata katiba Mpya nayo ina mchakato wake. Watunga na wapitisha hiyo katiba wanatakiwa wawe neutral la sivyo watajaza interest zao. Angalia hii Kamati ya Prof Mkandara linganisha na warioba ambaye hakuwa na vested interest katika katiba Mpya. Ona Kikwete alivyoharibu mchakato ule. Vijana tusiwalaumu hata sisi enzi za mtikila pale jangwani tulikuwa kama wao. Pascal unakumbuka?
 
🤔🤔🤔😤
 
Nakumbuka sana!.
Hili la mgombea binafsi, tumelipigia kelele sana humu!,
Kwanza tuliunga mkono juhudi za Mchungaji Mtikila (RIP) toka ile 2010 Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010
Tukalipigia kelele enzi za JPM Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!. haikusaidia kitu!.

Mama alipoingia tuu, tukapaaza sauti Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Kwa vile Mama ni msikivu, Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Let's hope for the best.
P
 
Kama Erythrocyte et al wangekuelewa, wangalijua kuwa JPM alikuwa mzalendo wa nchi hii maana hakulemba au kupindisha maneno. Upuuzi wa kumaliza hela zinazotakiwa kuleta maendeleo! Nani ajitie kitanzi? Nani aingize kichwa chake katika mdomo wa mamba? Samia apunguze madaraka yake kweli? Huyo atakuwa ni binadamu au fisi? Tume huru ili asiibe kura kweli na asaini hiyo kitu!!!! Ati matokeo yapingwe mahakamani akina Tindo wanashangilia wakati huo huo Samia anasema atagombea 2025! Hivi akili gani hizi Vijana wa chadema!!!!!!!! Mystery unaamini? Uliona jinsi ambavyo Rais wa USSR alivyokubali kujitia kitanzi aliishia hata kutozikwa na Putin. Unadhani Kikwete atakubali kesho aipate kama JPM alivyomsulubu! Mnatania nyie watu. Mbona hakuna anayezungumzia mgombea binafsi maana akina Zitto, Tundu Lissu na akina MBOWE wanajua hicho ni Kifo chao, Asali inayoyoma wakikubali mgombea binafsi!
Umenena ukweli mtupu
 
Mkuu kolola , naunga mkono hoja.
P
Ameweka wazi vikwazo vikuu na kwahiyo tunafanya ambayo hatuna haja nayo - ripoti zote kapuni bila kujali gharama zinazotumika.

Na kumbe wapinzani nao wanapenda katiba ya chama kimoja ya '77 ya bila mgombea huru. Haki ya msingi ya kuchaguliwa inaendelea kuminywa na kunyimwa!
 
Danadana !! Ukipiga danadana kwa muda mrefu ni lazima utakosea na mpira utadondoka chini !! Waulize wacheza mpira wa miguu kama nasema uongo !!
Labda ni mafundi wa freestyle football - danadana za bila kuangusha mpira! Hata akianguka mpigaji anaendelea kuzipiga kwa kutumia kila kiungo - kiuno, makalio, bega, miguu, visigino, magoti, nk.; na pengine hata kwa kwapa!
 
Hata Mwalimu Nyerere alilipigia kelele la mgombea huru (huru nzuri zaidi kuliko binafsi), akatolea mfano wa Sarwat (kama sikosei), aliyepewa fursa hiyo tena enzi za Chama kimoja - TANU
 
Ameweka wazi vikwazo vikuu na kwahiyo tunafanya ambayo hatuna haja nayo - ripoti zote kapuni bila kujali gharama zinazotumika.

Na kumbe wapinzani nao wanapenda katiba ya chama kimoja ya '77 ya bila mgombea huru. Haki ya msingi ya kuchaguliwa inaendelea kuminywa na kunyimwa!
Wapinzani wengi ni oppotunistics !! Japo sio wote !
 
Kwa ufupi sana; hii report ya prof. Mkandala ni usanii mtupu kwani lengo lake ni kwenda kufifisha mchakato wa katiba mpya na kuja na utopolo mwingine badala ya mwendelezo wa katiba ya Jaji Warioba!
 
Hata Mwalimu Nyerere alilipigia kelele la mgombea huru (huru nzuri zaidi kuliko binafsi), akatolea mfano wa Sarwat (kama sikosei), aliyepewa fursa hiyo tena enzi za Chama kimoja - TANU
Ninafarijika hapa JF kukutana na watu kama nyie. Wengi ni vijana haya mambo hawayaoni katika pande kuu nne. Angalia mifano ya nchi ambazo ziliandika katiba mpya ya maana, utakundua kuwa crafters walikuwa hawana maslahi na uongozi kwa kupenda au kwa kulazimishwa na sheria. Inatakiwa itungwe sheria kua mtu yeyote atakayehusika na uaandaaji wa katiba mpya au kupitisha, including Rais atakayesaini, asigombee uongozi wa nchi hii kwa muda wa miaka 20 ijayo. Hapo mtapata mnachokitaka. Zaidi ya hapo ni makelele tu
 
Back
Top Bottom