Ni lini mapendekezo ya Ripoti hizi yatafanyiwa kazi?

Ni lini mapendekezo ya Ripoti hizi yatafanyiwa kazi?

Wapinzani wengi ni oppotunistics !! Japo sio wote !
Ni kweli kabisa. Japo neno zuri kwa muktadha wa Kiswahili chetu na mtazamo wetu lingefaa litumike neno "washindani" (political competitors), badala ya. Wapinzani (political opponents)
 
Kwa ufupi sana; hii report ya prof. Mkandala ni usanii mtupu kwani lengo lake ni kwenda kufifisha mchakato wa katiba mpya na kuja na utopolo mwingine badala ya mwendelezo wa katiba ya Jaji Warioba!
Inasikitisha sana, tena sana!
 
Ninafarijika hapa JF kukutana na watu kama nyie. Wengi ni vijana haya mambo hawayaoni katika pande kuu nne. Angalia mifano ya nchi ambazo ziliandika katiba mpya ya maana, utakundua kuwa crafters walikuwa hawana maslahi na uongozi kwa kupenda au kwa kulazimishwa na sheria. Inatakiwa itungwe sheria kua mtu yeyote atakayehusika na uaandaaji wa katiba mpya au kupitisha, including Rais atakayesaini, asigombee uongozi wa nchi hii kwa muda wa miaka 20 ijayo. Hapo mtapata mnachokitaka. Zaidi ya hapo ni makelele tu
Hakika tunaumia tu na kufuja fedha za umma zinazohitajika sana kuleta maendeleo
 
Ameweka wazi vikwazo vikuu na kwahiyo tunafanya ambayo hatuna haja nayo - ripoti zote kapuni bila kujali gharama zinazotumika.

Na kumbe wapinzani nao wanapenda katiba ya chama kimoja ya '77 ya bila mgombea huru. Haki ya msingi ya kuchaguliwa inaendelea kuminywa na kunyimwa!
Niliyokuwa nayasema haya hapa jionee mwenyewe

 
Danadana zinaendelea na kuendelea kutafuna fedha za umma. Ya Nyalali yalitupwa, Kisanga alifokewa na Mkapa, Warioba akashambuliwa na Kikwete na hadi kupigwa ngwala na kijana wake Makonda ambaye alipewa zawadi ya ukuu wa wilaya ya Kinondoni.

Na huyu kaja na "si amri" - danadana zinaendelea!

Nyalali: Season 1
Kisanga: Season 2
Warioba: Season 3
Mukandala: Season 4
Nanihii (!?): Season 5
...tunasuburi
Hawalazimishwi.??
 
Back
Top Bottom