Ni lini serikali itaingilia kati huu wizi wa mitandao ya simu kuunganisha watu kwenye huduma wasizohitaji?


Wanadukua phone book ya Mtu,na sio kwamba anaweka Kama mdhamini
 
Yan hili suala la mitandao ya simu kutukata fedha limekuwa sugu. Tutafuteni suluhu. Nashauri jamii forum muongeze sehemu ya kuweka sauti tuwe tunawasilisha ushaidi juu ya mambo haya
 
Pia kuna zile "pop-up sms" za hio mitandao huwa zinajitokeza ghafla kwenye screen yako ya simu. Usikimbilie kubonyeza "ok" ili kuiondoa hio sms. Mda mwengine yanakuwa ni maelezo ya kujiunga huduma fulani. Ukibonyeza ok umejiunga rasmi
 
Takwimu za TCRA za 2022 zinaontesha kuna watumia milion 39.
Vodacom ina watumiaji 39% ya hao milion 39.
Kwamba vodacom ina wateja million 15.

Sasa basi, kuna huduma wanaweza ku push kwa wateja bila wao kujiunga na kukata Tshs 100.
Kwa mwingine hii sio kitu kabisa, anaona 100 ndogo ya nini kuhangaika.
Hizo 100 mia wakikata kwa wateja 800,000.Tayari wadau wanaingiza 80,000,000.kwa siku.
Hata kwenye bando ndio wanapiga sana.
 
duuuu
 
Vodacom wanatamani wananchi wote tujiunge na ile Voda bima yao iliyokaa kitapeli, ili watupige vizuri wananchi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…