Ni lini serikali itaingilia kati huu wizi wa mitandao ya simu kuunganisha watu kwenye huduma wasizohitaji?

Ni lini serikali itaingilia kati huu wizi wa mitandao ya simu kuunganisha watu kwenye huduma wasizohitaji?

Kuna watu wanakopa mtandaoni huko halafu wanaweka namba yako kama mdhamini... Siku anashindwa kulipa deni sasa wana anza usumbufu kisa namba ipo kama mdhamini..

TCRA na BOT iwadhibiti hawa watu... Nipate taarifa kwanza kuna mtu anataka niwe mdhamini... Nikubali mwenyewe ndio wakopeshane huko... Wanakopeshana wenyewe halafu usumbufu wanaleta kwangu... Hii haikubaliki kabisa... Wataoga lugha za maudhi tu.

Samahani mleta mada, nimetoka nje ya maudhui ya uzi wako

Kuna watu wanakopa mtandaoni huko halafu wanaweka namba yako kama mdhamini... Siku anashindwa kulipa deni sasa wana anza usumbufu kisa namba ipo kama mdhamini..

TCRA na BOT iwadhibiti hawa watu... Nipate taarifa kwanza kuna mtu anataka niwe mdhamini... Nikubali mwenyewe ndio wakopeshane huko... Wanakopeshana wenyewe halafu usumbufu wanaleta kwangu... Hii haikubaliki kabisa... Wataoga lugha za maudhi tu.

Samahani mleta mada, nimetoka nje ya maudhui ya uzi wako.
Wanadukua phone book ya Mtu,na sio kwamba anaweka Kama mdhamini
 
Yan hili suala la mitandao ya simu kutukata fedha limekuwa sugu. Tutafuteni suluhu. Nashauri jamii forum muongeze sehemu ya kuweka sauti tuwe tunawasilisha ushaidi juu ya mambo haya
 
Ni Jambo linakwaza sana. Unanunua vocha kujiunga na kifurushi unachopenda mara unapata ujumbe kuwa Salio lako halitoshi.

Unafuatilia unaambiwa umejiunga na huduma za kidijitali kama vile "afya call" ,"Tikisa ushinde" n.k.

Huna taarifa na huduma hizo,hujui umejiungaje na wala hujui zinahusu nini,ila pesa zako zinakwenda na kiendacho kwa mganga hakirudi.
Je serikali imebariki huu uhuni wa miaka nenda rudi unaofanywa na Vodacom na mitandao mingine ya simu?

Mbaya zaidi nimejaribu kujiondoa na hizo huduma nimeambiwa "Ombi lako la kujiondoa kwenye Tikisa Ushinde halikufanikiwa Piga *149*83# kujaribu tena."

Huu ni wizi kama wizi mwingine,nadhani ni wakati sasa suala hili likashughulikiwa ipasavyo.
Pia kuna zile "pop-up sms" za hio mitandao huwa zinajitokeza ghafla kwenye screen yako ya simu. Usikimbilie kubonyeza "ok" ili kuiondoa hio sms. Mda mwengine yanakuwa ni maelezo ya kujiunga huduma fulani. Ukibonyeza ok umejiunga rasmi
 
Takwimu za TCRA za 2022 zinaontesha kuna watumia milion 39.
Vodacom ina watumiaji 39% ya hao milion 39.
Kwamba vodacom ina wateja million 15.

Sasa basi, kuna huduma wanaweza ku push kwa wateja bila wao kujiunga na kukata Tshs 100.
Kwa mwingine hii sio kitu kabisa, anaona 100 ndogo ya nini kuhangaika.
Hizo 100 mia wakikata kwa wateja 800,000.Tayari wadau wanaingiza 80,000,000.kwa siku.
Hata kwenye bando ndio wanapiga sana.
 
duuuu
 
Vodacom wanatamani wananchi wote tujiunge na ile Voda bima yao iliyokaa kitapeli, ili watupige vizuri wananchi!!
 
Back
Top Bottom