Ni lini sisi wavuvi na wafugaji tutathaminiwa na kupewa siku yetu ya mapumziko?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Naandika kwa masikitiko makuu juu ya ubaguzi huu wa wazi wazi.

Wafanyakazi tulipumzika mei mosi, leo ni sikukuu ya wachuuzi tunapumzika, tarehe 8 August tutapumzika kwaajili ya wakulima, ni lini sisi wavuvi na wafugaji tutathaminiwa?

Hili jambo liingie kwenye Katiba mpya.
 
Huwa mnajumlishwa kwenye kundi la wakulima.Sikukuu ya "Wakulima-mseto"!😂😂😂😂
 
Hoja gn we unaongea mashudu hapa nimekuuliza we unafuga? Kwa sababu mi najua jinsi serikali inafanya kusupport wakulima, wafugaji na wavuvi huenda unazungumzia kitu hujui ndo maana nakuulza
Hizo ni assumptions zako
 
Hoja hii ipelekwe bungeni ipendekezwe siku moja wapo katika mwaka🤣🤣
 
Agriculture is the human activity which deals with crop cultivation and animal keeping. Geography Form 3. Nyie ndo mlikua mnaunguza wenzenu na mbegu za ubuyu darasani wakati mwalimu anafundisha.
Wavuvi je?
 
we akili umeikabidhi wapi, ufugaji na uvuvi ni sehemu ya kilimo. Acha uvivu tumia akili
 
Ni vile huna ratiba. Unapumzika sana wakati mifugo ikishashiba. Pia kama unafuga kisasa unapumzika sana tena sana. Wavuvi wengi wanavua usiku na mchana wanapumzika. Labda wewe unafuga na kuvua kwenye key board. Tofauti na mchuuzi akifungua duka saa 12 asubuhi anfunga saa 3 usiku amechoka mbaya. Hata leo sabasaba yuko kazini. Kikubwa hujajipanga ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…