Ni magonjwa gani yanayoua ghafla na dalili zake ni zipi?

Ni magonjwa gani yanayoua ghafla na dalili zake ni zipi?

Rebeca 83 kwani ukipima afya inazuia kifo, au nikukusaidia kufahamu ugonjwa?! Nafahamu unaweza kuwahi matibabu,lakini kifo hakikwepeki.

Mnh mkuu ni sawa na kusema tunaenda hospital kufanya nini,Kama kifo kipo tu,,yes ukipima ugonjwa na kujua uta adjust your life labda kwa kuanza kutumia medications na hivyo kuendelea kusurvive
 
Wakati mwingine ni kupaliwa na chakula,hususan wali...minishaponea chupuchupu mara mbili nashituka ghafla usingizini na kukuta pumzi ikikatakata
 
Doh!
kwa kuwa hutokea wakati umelala ,upo kwenye usingizi mzito hakuna cha warning sign,yaani unajikuta umeshakufa.
ila kwa hiyo rupture brain aneurysm inaweza tanguliwa na maumivu makali ya kichwani yanayoweza kukushtua toka kwenye usingizi ,lakini napo utakosa nguvu za kufanya chochote hivyo kufa. Hiyo kushuka kwa sukari mara nyingi utanguliwa na kutoka jasho jingi ,lakini kwa vile upo kwenye usingizi unawez usihisi chochote hivyo unajifia zako polepole kwenye usingizi
 
Mnh mkuu ni sawa na kusema tunaenda hospital kufanya nini,Kama kifo kipo tu,,yes ukipima ugonjwa na kujua uta adjust your life labda kwa kuanza kutumia medications na hivyo kuendelea kusurvive
Hahaha maana yangu ilikuwa hiyo, kifo hakizuiliki, naona watu hufia hospitali pia. Labda unataka usiwahi kufa, lakini kifo hakizuiliki.
 
Nilikua namaanisha hakuna dalili kuwa una ugonjwa huu,hivyo nenda hospital ?kwa maana nyingine ugonjwa unatokea hapo hapo na kifo kinatokea hapo hapo? 😣🙄😇😇
Nimekuelewa apa kuna makundi mawili, kundi la kwanza ni lile la wagonjwa wenye matatizo ambayo yanajulikana tayari kwa mfano shinikizo la damu na kisukari,hawa wanakuwa kwenye hatari ya kupata shida hizo za kuzimika ghafla ikiwemo wakati wakiwa wamelala usiku.Kwa mgonjwa wa namna hii anayefata ratiba yake ya kwenda kliniki na kufata maagizo toka kwa daktari wake anapunguza uwezekano wa kupata complications ikiwemo vifo vya ghafla.
Kundi la pili ni la watu wenye matatizo ya magonjwa lakini wenyewe hawajijui ya kwamba ni wagonjwa tena magonjwa makubwa.Yaani unawez kuta mtu ana tatizo la high blood pressure au kisukari lakini yeye hajijui,hii ni kwa sababu aya magonjwa ya tabia ya kukutafuna polepoe kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili yoyote(chimbuko la jina la silent killer).Hivyo basi mtu wa namna hii anaweza akakumbwa na kifo cha ghafla ikiwemo wakati wa kulala, ndiye ile unaanza kusikia jamani fulani si alikuwa mzima tu, kumbe kiuhalisa alikuwa anashinda ambayo ilikuwa haijajionyesha.
Ukweli wa chanzo/sababu ya vifo vya ghafla au usingizini ubainika kwa kufanya postmortem na apo ndio inabaainika unakuta damu imevuja kwenye ubongo,moyo ulikuwa mpana etc , ingawaje kwa baadhi ya watu postmortem inashindwa kubaini sababu ya kifo kwa muhusika
 
Ukikamatwa huko kwenye ndoto yaani ukiwa kwenye ndoto halafu ndani ya ndoto mtu akakushikilia au kuzuia usistuke kutoka kwenye ndoto na kurudi duniani au kwenye mwili au kuamka ndo unapitiliza ikifika asubuhi tayari maiti. Wakati hukuwa na ugonjwa wowote ule.
Mkuu unataka kutuambia kuwa mtu akilala nafsi huuacha mwili, hafu inaenda kujoin na watu wengine huko , na inaweza kukamatwa na kuwekwa lupango ya huko, basi kama ndo hivyo wanaochelewa kuamka huenda wanakuwaga na misala ya kuwekwa sero.
 
Back
Top Bottom