ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Kwa wale ambao mmepata neema ya kuwa na mama Mpaka sasa Hivi ni mambo gani haupo comfortable kabisa kuzungumza na mzazi wako labda itokee yeye aanzishe. Mimi binafsi yako mengi ila.:-
1.Siwezi kupiga picha na mama ya pamoja labda itokee bahati mbaya tumepiga ile ya familia pamoja ila sisi mimi nimwambie mama eti tusimame tupigwe picha duh na Kosa kumbukumbu muhimu.
2.siwezi kumkumbatia mama yangu hata kama hatujaonana miaka miwili. Mama zangu wadogo na mashangazi Sawa tukikutana nao kama ni siku nyingi tunakumbatiana ila sio mama eti waooo waooo.
3.kuzungumzia kuhusu mchumba ambaye atakuwa mke.. Kama unavyojua ujana huu sometimes unampata mtu ukiamini utakuwa naye kabla shetani hajaingilia Kati mkaachana kama lilivyo lengo la mapenzi ya siku hizi ni kuachana. Sasa mimi ile hoja ya kwamba naishi na fulani ni mtu wangu aisee siwezi kumwambia mama nitakachofanya ni kuwatumia mama wadogo au kina bibi nikiamini Habari zitamfikia bi. Mkubwa na yeye atakuja kuniuliza kisha nitamwelekeza ila sio mimi kumuanza kumwambia.
4.kingine siwezi kumpa pongezi mama iwe ni siku yake ya kuzaliwa, au siku ya wanawake au siku ya wamama yoyote ile siwezi kuwa na uthubutu wa kuandika mama nakupenda sijui blah blah huwa nashangaa mtu Ana post kabisa picha akiwa na mama yake kwenye mitandao.