Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Ndugu yangu alimkuta mchungaji na mke wake wanaroga kanisani (alikua anaenda ibada ya usiku - walokole) walivomuona wakamwambia usije kanisani hadi zipite siku 7 na usimwambie mtu yeyote haya uliyoyaona hapa, akahisi wanatania.

Kesho kutwa yake alienda kanisani (ilikua ijumaa wanakati wanaroga, jumapili akaenda ibada ya jumapili), alivotoka kanisani akawa mwehu ghafla, akawa anakimbia kimbia tu hadi akaanza kusahau watoto, akafungwa kamba na kuanza kuombewa (mme wake alikua hajui chanzo ni nini). Wamehaingaika nae kwa muda mrefu, ikabidi apelekwe kwa waganga wa kienyeji, alikuja kupata unafuu baada ya miaka miwili mbele ndiyo kusimulia yote.
Mtu kapigwa uchawi kanisani kaponea kwa mganga wa kienyeji

Makanisa haaayaaa
 
kutoka misr kwenda kanaan walibeba mifupa ya Yusufu.Je Yusufu alozikwa wapi? Uvumba ni kitu gani? Acha wazike tu maana ya biblia nayo ni mengi ukiachana na ukristo ambao wengi wanadhani katiba yake ni biblia .Katika imani mengine tujiongeze tu tunaenda .kitimoto ni haramu kwann wana wa Israel waliwafuga?kwanini nguruwe mpaka leo wapo? Kuna miujiza Yesu anafanya mingine anakupaka tope alilofanya kwa mate yake na mingine anasema tu inuka au ona .kwann yote asiseme ona ,tembea .kuwa na imani mdau hata hirizi biblia haikatai .Usinzi tu inategemea mbona Daud alizini nq hakupigwq mawe? Kuna wakati Musa aliua.Yoshua aliua na wanafunzi wa Yesu waliua pia au wewe usomagi biblia ? Unaambiwa hata shetan atauwawa kwa pumzi ya Yesu yaani hata Yesu mwenyewe anaua haah sembuse mimi ?na huko mbinguni kuna vita vinapiganwa yaani hata mbinguni kuna mmama amezaa just image hiyo mimba kama sio ya usinzi n nani aliifungisha hiyo ndoa maanq imeandkwa mbingun hawaoi wala kuolewa.Tafakar ndg .notes mimi sio muislam wala chawa.
 
Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali ~chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa~ kuwa msimamizi wa kanisa

Labda mimi sijaelewa sio mifupa ila ni chembe chembe ndogo za aliyekufa
Hakuna lugha ya mifupa bali masalia.
Labda kiingereza kina maana nzuri zaidi "remains"
 
Ndugu yangu alimkuta mchungaji na mke wake wanaroga kanisani (alikua anaenda ibada ya usiku - walokole) walivomuona wakamwambia usije kanisani hadi zipite siku 7 na usimwambie mtu yeyote haya uliyoyaona hapa, akahisi wanatania.

Kesho kutwa yake alienda kanisani (ilikua ijumaa wanakati wanaroga, jumapili akaenda ibada ya jumapili), alivotoka kanisani akawa mwehu ghafla, akawa anakimbia kimbia tu hadi akaanza kusahau watoto, akafungwa kamba na kuanza kuombewa (mme wake alikua hajui chanzo ni nini). Wamehaingaika nae kwa muda mrefu, ikabidi apelekwe kwa waganga wa kienyeji, alikuja kupata unafuu baada ya miaka miwili mbele ndiyo kusimulia yote.
Nimecheka sana.
 
Hii siyo hadithi wala story ni mwaka huu tu imetokea kwenye kanisa langu la siku zote.

Basi kulikuwa na usimikaji/kuzindua kanisa jipya tulilo changa ma hela kwa miaka kadhaa hadi mwaka huu likawa limekamilika na hatimae Askofu alikuja kulizindua kanisa hilo pamoja na kupewa hadhi ya kuwa parokia

Jambo lililo tuacha midomo wazi waumini wengi ni mambo kadhaa wa kadhaa (sita yataja yote) tukio la kulisimika kanisa lilianza saa3 asubuhi hadi saa10 jioni.

Moja ya matukio tuliyoona kwa macho ni mifupa ya marehemu aliye fariki siku nyingi kuletwa na kuzikwa kweye arutale(mimbari) Huyu marehemu ambaye kwa sasa tunamuita MT fulani kwa imani yetu.

Kulikuwa na chungu kama vile vya waganga wa kienyeji na vilikuwa na vitu kadhaa mle ndani pamoja na mkaa wa moto huku moshi mzito ukifuka.

Baada ya yote hayo kuisha kiongozi wetu wa dini yaani (.....) alipapaka mafuta na kuanza kupasugua na kupasafisha yeye mwenyewe. Na mengine mengi.

Hakika kwa haya yameniacha mdomo wazi na sio mimi tu nimejaribu kuuliza viongozi kadhaa wa dhehebu langu sijapewa jibu la kueleweka maana mimi niliona kama ni kinyume na ukristo.

Wakuu nahitaji kuuliza maana nilijua najua vitu vingi kwenye imani yangu kumbe bado kabisaaa ni mtoto.je hii ina ulazima gani na kwanini ifanyike hadharani na mc akitangaza hadharani kwenye vipaza sauti na watu wasio sali dhehebu letu wasikie na kujua kinacho endelea?

Je, wewe umewahi kuona kitu ambacho kilikuacha mdomo wazi na maswali mengi .
Poleni...
 
Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali ~chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa~ kuwa msimamizi wa kanisa

Labda mimi sijaelewa sio mifupa ila ni chembe chembe ndogo za aliyekufa
Eeh chembechembe si ni ndogo!?. Ni kama mkato wa kucha hivi ama hata vuzi au kinywele O🤪
 
Religion and witchcraft depends on who is doing it.

Kinacho fanyika makanisani hakina tofauti na wanachofanya waganga na wachawi.

Wakatoliki watakushangaa kusali makaburini kwa mababu zako, Lakini hawajishangai wao kusali kwenye zege lililosimamishwa kama sanamu ya bikira Maria na Yesu.
Mnavyopanda ndege kwenda kwenye lile tofali pale maka huwa mnaakili au matope kichwani?? Yaani wewe na ukoo wako wote mnaenda kulia kwenye jiwe jeusi la kimondo?..........lile kaburi pale la jamaa wa kuitwa mudi......nyie mnatoka kira sehemu hapa duniani kwenda kwenye jiwe jeusi ........si muende mbeya lipo wanaliita kimondo
 
Umezunguka sana lakini hapo unamaanisha RC.
Kwanza hakuna kitu kinachoitwa kusimika au kuzindua kanisa.Na masalia yanayowekwa sio ya muanzilishi wa kanisa maana muasisi wa kanisa ni Yesu mwenyewe alipomuambia Petro ya kwamba atalijenga kanisa lake juu yake.

Tukio unalosema ni kutabaruku kanisa.Maana yake ni kuliweka wakfu jengo hilo na kulitenga mbali na shughuli nyingine za kidunia/kijamii ili litumike tu kwa ajili ya sadaka ya ibada takatifu ya misa.

Ubani unawekwa katika chungu na kufukizwa juu ya altare (meza ile ya kutolea dhabihu)ishara ishara ya kupatakatifuza na kumsihi Mungu ya kwamba sadaka zitakazotolewa hapo zipae kwake juu na harufu nzuri ya kumpendeza kama moshi huo wa ubani.Kadhalika husuguliwa kwa mafuta matakatifu ishara ya kupatakasa.

Unayosema mifupa ililetwa sina hakika kama uliiona mifupa kwasababu huwa sio mifupa haswa bali chembe ndogo sana ya masalia ya huyo mtakatifu aliyewekwa kuwa msimamizi wa kanisa mahalia.Kwa imani yetu sisi wakatoliki watakatifu wanao uwezo wa kutuombea kwa Mungu ndio maana tuna litania ya watakatifu.Hivyo kuweka alama yake katika kanisa husika ni ishara ya kukabidhi usimamizi wa kanisa husika kwake.

NB kwa maelezo ya mleta mada ninathubutu kusema sio mkatoliki maana naona hajui kila kitu.
"Chembe ndogo za masalia ya huyo mtakatifu"- Mwisho wa kunukuu.
 
Mnavyopanda ndege kwenda kwenye lile tofali pale maka huwa mnaakili au matope kichwani?? Yaani wewe na ukoo wako wote mnaenda kulia kwenye jiwe jeusi la kimondo?..........lile kaburi pale la jamaa wa kuitwa mudi......nyie mnatoka kira sehemu hapa duniani kwenda kwenye jiwe jeusi ........si muende mbeya lipo wanaliita kimondo
Mimi sina dini ya aina yeyote ile.

Sasa punguza mihemko yako kudhani kila mtu ana udini.

Ukristo na Uislamu zote ni UTAPELI.
 
Back
Top Bottom