Kuna ishu zingine bana kusamehe ni kama vile kimeo imagine mwanamke anayepigwa na mumewe kila siku hapo unaweza kuwa unasema unamsamehe mtu mumeo .
Ubakwe halafu useme usamehe?? Tatizo ni yale makovu yanayokuwa ndani imagine kila siku unakutana na huyo mbakaji wako how would you feel?? Hapo sidhani kama msamaha utafanya kazi
Ngoja nianze na wewe ili nikamalizie na Lizzy.
Kuna pande mbili za haya mambo........Mtu akikukosea, akitambua kuwa amekukosea, akakuomba msamaha, maana yake amegundua alililotenda kuwa si jema kwako hivyo anakusudia kutokufanyia tena. (hapa haijalishi ukubwa wa tendo/kosa. Lakini makosa yapo ya aina mbili......amabyo mkosaji anakuwa amekukosea wewe tu, na hakuna hatari ya kuwa ameikosea jumuiya inayokuzunguka, au amekukosea wewe na jumuiya nzima au ni hatari kwa jumuia inayo mzunguka. Mfano, cheating is more personal, Kuiba is swala la jumuia zaidi, au kubaka ni jambo la jumuia zaidi......inampasa mkosaji aiombe radhi jumuia, na kwa kuwa sio rahisi, na jumuia imejiwekea utaratibu wa kuishi, basi huyo mtu anatakiwa aondolewe kwenye jumuia hiyo.
Now: Kama mume au mke anakutwanga kila siku, huwezi kusema simsamehi au namsamehe........ukisamehe unaendelea kula kichapo usiposamehe unakula kichapo vile vile.......Hili sio jambo la msamaha ukiwa ndani........toka kwenye mahusiano hayo, then samehe na endelea na maisha.
makosa mengine yanajadilika.....kama mtu ana-cheat na anaomba msamaha na maisha yanaendelea bila tukio jingine sasa ugonvi wa nn.
Swala la MSAMAHA ni jambo ambalo ni discussion kubwa among wanawake.........hasa kwa makosa yanayoumiza hisia zao, ni wagumu kusamehe. NDIYO ni wagumu kusamehe.......na hawasahau. Kuchanganya msamaha wa makosa makubwa kama kuua mtoto na cheating inaonyesha wazi ni kwa jinsi gani hisia za wanawake zilivyo na thamani kwao kuliko tunavyoweza kufikiri.
ILA KUSAMEHE NI KAZI NGUMU NA AMANI ITOKANAYO NA MSAMAHA NI AMANI ILIYO KUU. HUWEZI KUISHI KWA KUTOSAMEHE or at least KUSAHAU basi.