brokenagges
Member
- Sep 29, 2022
- 58
- 33
sidhani kama kuwa na leseni ya duka ama biashara ndo inampatia mtu uhuru wa kutumia barabara kwa matumizi yake binafsi na kwa namna anavyotaka yeye bila kujali wengine wala kufuata sheria na taratibu za amtumizi ya barababra.
Inakuwa ni rahisi sana kama picha inavyoonyesha uwezekano kugongwa watembea kwa miguu ama kugonga kwa wenye vyombo vya moto unakuwa ni mkubwa sana.
ni vizuri zichukuliwe hatua za kuepusha ajali kabla ajali haijajitokeza.
Barabara hii ilikuwa ni kero sana kipindi machinga waliporuhusiwa kufanya biashara eneo lolote la barabarani bila kujali na baadae machinga walipoondolewa eneo hili likawa liko sawa.
ila sasa kero ya machinga imeonekana kwamba haikuwa kero kubwa kama hila la kupaki gari kama Canter kukatiza barabara katikati mjini na kama tunavyofahamu ufinyu wa barabara zetu za katikati ya miji.