msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Nianze na suala la kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani bw. Freeman Aikael mbowe
kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani kwa tafsiri ya kisiasa inaweza kuonekana ni agizo kutoka juu ili kudhoofisha upinzani au kukwamisha mapambano ya kudai katiba mpya.
Lakini ukweli ni kuwa kukamatwa kwa mbowe ni uamzi wa jeshi la polisi chini ya IGP sirro ndio maana kwenye hotuba ya juzi mheshimiwa Rais alimsisitiza sana pamoja na mifumo ya utoaji haki yaani 'mahakama' na 'DPP' kufuta kesi na mashauri yote ambayo hayana ushahidi wa kutosha kwani haya mambo yote kwa ujumla wake yanaidhalilisha serikali na kumchafua Rais na kwakuwa jambo lenyewe limeshafika mahakamani, Rais hawezi kuliingilia kwahiyo tuiache mahakama ifanye kazi yake na haki itatendeka.
Suala la kodi ya majengo
kodi ya majengo huwa ipo wala haijaanzishwa na mheshimiwa Samia. Kilichobadilika ni namna tu ya kufanya malipo. kwamba badala ya kulipa kwa mkono 'cash' kwa sasa tunailipa kidigitali kwa mfumo wa LUKU. Na, huu mfumo wa LUKU ni mzuri kwa sababu unasaidia kupunguzia wananchi mzigo kwamba badala ya kulipa 12, 000 au 60, 000 kwa mkupuo kwa sasa tuna lipa kwa kukatwa kidogo kidogo kwa mwezi. Pia mfumo huu unasaidia kupunguza hadha ya watu kusafiri umbali mrefu kwenda ofisi za TRA kufanya malipo. Vilevile unasaidia kudhibiti ukwepaji kodi kwa watu ambao sio waaminifu na wazalendo.
Tozo ya miamala ya simu
Mheshimiwa Rais anajua kazi nzito iliyoko mbele yake. Anajua kuna miradi mikubwa iliyoanzishwa inahitaji kuendelezwa, anajua watumishi wa umma wamenyimwa haki yao ya kupandishiwa mishahara kwa kipindi kirefu, anajua kuna changamoto katika huduma za afya na elimu, anajua kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana. Lakini changamoto zote hizi atazitatuaje bila ya kuwa na pesa?
Ndio maana kwa mapenzi mema, mheshimiwa Rais pamoja na serikali yake wakaamua kuanzisha kodi ya kizalendo 'solidarity fund' kupitia miamala ya simu ili pesa itakayopatikana ikasaidie kutatua changamoto hizo lakini bado watu wanalaumu? HAPANA tumpeni muda Rais afanye kazi na matokeo tutayaona.