Ni mapema mno kumnyooshea kidole mheshimiwa Rais, Tumpe muda!

Usisahau kuwa na Mama anamuunga mkono au niseme anaig'arisha sana Zanzibar. Si umesikia kero zaidi ya 10 zimepata ufumbuzi ndani ya muda mfupi
 
ACHEN KUMDEKEZA

MPE MUDA MPE MUDA NN???

HUYO NI MTI MZIMA ANA AKILI TIMAMU.


HAFAI, HAFAI NA HAJAWAHI KUFAA KUA RAIS.



2025, VYOMBO VYA DOLA, KAMA MMESHINDWA SANA KUACHA WANANCHI WACHAGUE, BASI MSITULETEE MTU WA AINA HII KUPITIA CCM.
Shangwe la wakulima wa mazao mbalimbali baada ya bei kupaa ni kwa mama tu.Hayo ya ujinga wa kina Mbowe bakini nayo nyinyi washikiwa akili.
 
Usisahau kuwa na Mama anamuunga mkono au niseme anaig'arisha sana Zanzibar. Si umesikia kero zaidi ya 10 zimepata ufumbuzi ndani ya muda mfupi

Ni kweli, lakini tangu wakati wa JPM mentality, speed yake ilikuwa hiyo hiyo. Mchaka mchaka. Hata angekuwepo JPM sidhani kama angekuwa tofauti, labda speed zaidi.

Yale yanayofanyika Zenji yangeweza na yanaweza kufanywa bara kama Mwinyi angekuwepo huku.

It should be win-win situation for both countries. Kuna keki kubwa tu ya kutosha na maslahi, rasilimali, interests, na uchumi unaotegemeana.
 
Kodi ya majengo imewalenga wanaotumia umeme kupitia TANESCO, je wale wanaotumia solar na wale wa karabai, vibatari, kandiri n.k. wanalipiaje majengo yao?
 
UPUUZI MTUPU!
 
Namuelewa sana MAMA, ila anahitaji kufumua safu ya juu ya uongozi kwa baadhi ya vyombo vyetu vya ulinzi...wanamuangusha na hajui
Hana ubavu huo. Hao ndiyo wanamfanya aendelee kubakia madarakani. Akiwagusa itakula kwake
 
Kuna msemo usemao "mvinyo mpwa kwenye chupa ya zamani"."New wine in old bottle".hicho ndiyo kinachoendelea awamu sita Hawa wasaidizi wa Rais ni vigegeu,bendera fuata upepo na hawana misimamo, watamuangusha. Mama awe mwangalifu Sana,hawamtakii mema.
Ambao wanakwamishwa awaweke pembeni ili kazi iendelee.
 
Huu ni upuuzi wa kiwango cha juu sana.
 


Wewe ndio President, Commander in Chief, final decision maker with tremendous exucutive power. Kwahiyo unatakiwa uwe na uwezo wa kuamua ushauri gani uuchukue, upi uuache.

Unapokea ushauri, mapendekezo. Kazi yako uliojiriwa na Watanzania ni kutoa maamuzi ya mwisho. Hicho ndicho kitu kikubwa, kuisimamia serikali yako, kuamua.

Sasa kila siku unasikia wasaidizi wanamkwamisha, wanamuhujumu, wanamyumbisha,hawana msimamo.

Wao wanafuata msimamo wa Rais wao. Kama ya Rais amesimama na wao watasimama au kusimamishwa.

Kama anayumba na wenyewe watayumba. Unafikiria wanafanyaje maamuzi kama haya kodi na tozo mpya nne kwa kipindi cha miezi miwili zinazogusa directly vitu na huduma muhimu kwa Jamii.

Kweli hatuna ubunifu, wa kuongeza mazao tunayolima, kutumia vifaa na mbinu za kisasa, kuzifanya balozi zetu kazi yao kubwa kabisa kuwa kutangaza utalii, bidhaa zetu, madini, kutafuta masoko, fursa zinazopatikana nchini za kibiashara, uwekezaji.

Hapo naona balozi wa China na Comoro wanajitahidi wengine hatusikii chochote. Inabidi kuchagua Mabalozi wemye weledi na kuwapa maelekezo kazi zao ni zaidi ya kuimarisha mahusiano.
 
Kodi ya majengo imewalenga wanaotumia umeme kupitia TANESCO, je wale wanaotumia solar na wale wa karabai, vibatari, kandiri n.k. wanalipiaje majengo yao?
Wanaotumia solar wanalipa kupitia benki au kwa njia ya mtandao kama m-pesa, tigo-pesa n.k
 
Bonge la pambaf
 
Kodi ya majengo imewalenga wanaotumia umeme kupitia TANESCO, je wale wanaotumia solar na wale wa karabai, vibatari, kandiri n.k. wanalipiaje majengo yao?

Watatumia mfumo wa zamani obviously. Naipongezwe hii mbinu ya ukusanyaji kodi, kinachotakiwa ni maboreshe na kuhakishi mpangaji asiye na nyumba na wenye exception wazee halipishwi, hivyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…