Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Sijawahi aga naenda wapi wala nitarudi lini au saa ngapi? Ko hata mechi za ugenini zinaponea humo!

Ni mwiko kuniuliza nilikuwa wapi au nimetoka wapi Ko mi hata saa nane usiku nitarudi/kutoka kwangu hilo halina mjadala alishazoe nirudi home nisirudi ye hana noma simu yangu ni mwiko kuishika au kuhoji ulikuwa unaongea na nani?
Kazi anayo aisee
 
Wangu jamani uwii! Ukikosea analisema jambo kama lilivyo bila hata chembe ya kupepesa macho.

Which is good, but kuna mambo huwa anakosea nashindwa kumface kumchana nampotezea tu nikiamini anajua anachofanya, ila ikija upande wangu nachanwa chanwa bila kuremba kitu. Sasa naona why mimi nambebea madhaifu yake yeye hanibebei? Is it fair?

Ukisafiri ukiwa unarudi lazima alazimishe kuja kukupokea, yaani hii ni lazima sio ombi, tatizo ni kwamba hata umwambie nusu saa kabla hujafika, au lisaa kabisa lazima achelewe, yaani lazima achelewe. Kwahiyo mimi kukaa airport/Au stendi dakika 10/15/20 ni kitu cha kawaida tu. Nilishamshauri hili suala la kunipokea aliache, ntapanda tax, bajaji etc ila hakubali ng'oo ni bora umuue! Nishanuna sana, nishazira sana ila haisaidii. Mwaka wa 9 huu.

Anyways.... Naishi humo!
Unataka kauhuru flani hivi, ukishuka Airport uwe huru kuchagua aina ya usafiri unataka, ila shukuru kwa kumpata wa namna hiyo, he cares! Binafsi pia nampokea, ila kwa kuombwa, yaani siwezi kwenda kwa Magufuli bila yeye kuniomba.
 
Wakuuu habari za usiku.

Moja kwa Moja twende kwenye maada. Mimi kwa upande wangu mapungu yafuatayo kitoka kwa mama watoto wangu nimekubali KUISHI NAYO.

1. Kuto pokea simu.
Mke wa Mimi hapokei simu hata aione inaita hataahughulika NAYO Hadi amalize shughuli zake. Ukimpigia simu asipo pokea usijisumbue kutuma sms,ukituma Kuna siku utaisoma mwenyewe.

2. Dawa ya mswaki.
Kwenye matumizi ya hii KITU yeye huminya popote pale.

3. Hajichanganya na WATU.
Yeye ni kazini,nyumbani na kanisani. Haendi tofauti na maeneo hayo labda kwenye mambo ya jamii.

4. Ukimkosea hakiulizi na haoneshi kama amechukia ila utaulizwa siku nyingine na atawasilisha kwa njia ya utani.

5. Akikukosea ukiuliza atakuambia nisamehe baba......... hapo hata uongee vipi hatakujibu.
Hapendi kabisaa kijichanganya na WATU hasa ukitaka umuudhi fika nyumbani Anza kumwongelea mtu hapendi kabisaa na anachukia kwa dhati.

Haya ndo baadhi ya mambo ambayo nimeamua KUISHI NAYO na nimefamikiwa KUISHI NAYO kwa muda wa miaka 19 ya ndoa yetu.
Je anakagua simu yako?
2: mnapiga stories mkiwa home au ana gubu.
 
Sijawahi aga naenda wapi wala nitarudi lini au saa ngapi? Ko hata mechi za ugenini zinaponea humo!

Ni mwiko kuniuliza nilikuwa wapi au nimetoka wapi Ko mi hata saa nane usiku nitarudi/kutoka kwangu hilo halina mjadala alishazoe nirudi home nisirudi ye hana noma, simu yangu ni mwiko kuishika au kuhoji ulikuwa unaongea na nani?

Nilichoshindwa ni kumuita mama flani siwezi
Namuita kwa jina lake alishazoea po pote pale
Mkuu siku utapata matatizo huko, yeye atahisi ni kawaida yako either kutokurudi home, yaani mkeo asikuulize umetoka wapi uchelewa bila taarifa, mbona ubabe sana🤔
 
Kazi anayo mwanamke mwenzetu,mim hapa nilipo nabaki hapa hapa aisee hakuna marafiki ni sisi tu mi na yeye tu
Sipendi mwanaume anashinda na marafiki muda mwingi wana kunywa pombe au kuzurura hovyo
Pashikilie shoga, maana hali sio ni kupelekwa kama ng'ombe usiulize mume alipo usishike simu yake akirudi saa tisa poa tu
 
Back
Top Bottom