Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?


Ukiona kaacha kukupa umbea!! Sign kubwa sana, kuna mahali anapeleka na akimaliza kuthimulia tu......!!!
 
hahahahah
Kuna mda huwa naziba masikio anatuma kama sipo eneo hilo😁😁
Nshapokea sana malalamiko yake kwamba namtuma sana yani baba #%='¥$¢ kama muhindi, nikamkanya akawa hasikii sasa nikaamua kuacha kumtuma yeye nikaanza kuwa namtuma beki tatu kila kitu. Matokeo yake akisikia tu naita jina la beki tatu yeye huwa anajiwahi unataka nikuletee nini baba #£&@¥€? Naona kama adabu imeanza kumrejea.
 
Upo vizuri Mungu akubariki
 

Nimesoma weeee....! Sijaona mtu anayekabiliwa na mapungufu ninayokabiliana!!

Nimeoa msichana mzuri, tulikuwa tunafanana tabia kama kupenda kusikiliza aina fulani ya music pamoja. Kutoka outing, kupiga wine zetu wenyewe daaah!! Tukisafiri itaandaliwa collection ya music na humo garini ni raha tupu.

Sijui kakutana na mitume gani pumbafu!! Wamemfanya amebadilika totally, amekuwa mwoga wa maisha, anaogopa kufa kama yeye ndo atakufa pekee.

Nyumbani!! Hakuna kusikiliza music ni dhambi, no wine no anything!! Nyumba ipo kimyaaa....!!

Hakuna utani hakuna stories muda wote ni kuomba na kulia mpaka namshangaa kilichomkuta!!

Hakuna kujipodoa wala kusukia nywele bandia, dhambi!! Kuna manguo yao kama sketi za charanga yaan!! Kawa kama bibi fulani hivi!

Muda wote ni serious! Mkali kwa watoto mkali kwangu japo nilishamuwasha kwangu mie haleti ujinga wake.

Imebidi niwashike watoto (nipo nao close) maana niliona wanakuwa victims kwa hii tabia iliyokuja. Naye nimemuacha ajiendeshe mwenyewe kwanza akirudi kawaida tutaelewana.

Maisha nimeamua kuyafanya kama naishi alone kwanza ili mambo yaende ila ni kero kubwa saaana!!
 
Huyu ni mzungu na msomi hongera sana kwa kumpata huyu
 
Na. 1 sio nzuri
Kuna simu za dharula,aache ujinga!
Mfano ,mume kapata tatizo ye ndo anapigiwa afike kwenye tukio Kwa wakati na hapokei inakuwaje hapo?
No. 3 ndo km mi,aah mi sipendi bwana ,ila Huwa hatueleweki.
Ongea nae,mengine sio issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…