Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Bora wewe unajibiwa asante baba, wengine ni wanabisha hawajakosea na wako sahihi.. [emoji1787][emoji23]

Ukishinda hoja utaambiwa basi yaishe.

Nina mwanangu ana majanga, wakati mwingine unaona hata aibu kumtembelea nyumbani kwake.

Mkewe ana kaujeri kakimya kimya, ukimuona ni mpole lakini ni mjeuri kinoooma, mwanangu anapata tabu saana, kuna muda anafikiria kumuacha.

Mie wangu ni kutaka kujua kila kitu in details, ananiboa saana, chochote kile atataka in details, hata apige simu mtu akuongeleshe atakuuliza nani huyo, ndio yupi. [emoji23][emoji1787] Unamuliza utamjuaje sasa, hata nikikutajia fulani huwezi kumjua [emoji23], sijui ni kupenda kuongea na simu au vipi

Hata umpelekee zawadi atataka kujua yoote, kama umekopa, umemnunulia na sh ngapi, unajiuliza we unataka kujua nini, yaani ni shughuli pevu [emoji23]

Kingine anapenda mnoo kuongea na simu, bora muwe karibu hii inasaidia, akiwa mbali anapiga simu ataongea mpaka stori zaitaisha, mie mvivu kubonga na FONI naishia kuweka loudspeaker tu.

Sometimes hana stori, anakupihia anakwambia mwanao anakuita, sasa mtoto Mwenyewe ndio bado hajatimiza mwaka vizuri, kuongea haongei, unajua tu hapa nimemisiwa.

Mengine madogo madogo, yanachangiwa na maisha yangu ya awali.

Elewa neno AWALI. lizingatie vema.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hapo kwenye in details, amekuwa shushushu
 
Wakuuu habari za usiku.

Moja kwa Moja twende kwenye maada. Mimi kwa upande wangu mapungu yafuatayo kutoka kwa mama watoto wangu nimekubali KUISHI NAYO.

1. Kuto pokea simu.
Mke wa Mimi hapokei simu hata aione inaita hatashughulika NAYO Hadi amalize shughuli zake. Ukimpigia simu asipo pokea usijisumbue kutuma sms, ukituma Kuna siku utaisoma mwenyewe.

2. Dawa ya mswaki.
Kwenye matumizi ya hii KITU yeye huminya popote pale.

3. Hajichanganya na WATU.
Yeye ni kazini, nyumbani na kanisani. Haendi tofauti na maeneo hayo labda kwenye mambo ya jamii.

4. Ukimkosea hakuulizi na haoneshi kama amechukia ila utaulizwa siku nyingine na atawasilisha kwa njia ya utani.

5. Akikukosea ukiuliza atakuambia nisamehe baba......... hapo hata uongee vipi hatakujibu.

Hapendi kabisaa kijichanganya na WATU hasa ukitaka umuudhi fika nyumbani anza kumwongelea mtu hapendi kabisaa na anachukia kwa dhati.

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo nimeamua KUISHI NAYO na nimefamikiwa KUISHI NAYO kwa muda wa miaka 19 ya ndoa yetu.

1. Mbishi, anajibizana bila kuogopa

2. Hapendi kufokewa ila yeye analazimisha kufokewa kutokana na ubishi wake.

3. Anapenda kulia kuonesha kuwa kaonewa huku ndio yeye anasababisha

4. Upangilio wa nyumba na usafi kwa ujumla, anaweza kuacha kitu hakiko kwenye mahala pake kwa muda siku kadhaa, hadi umwambie ndio anakiweka mahali pake.

5. Nikiwa naye public anapenda kujionesha kuwa ana mume kwa kuniita ita(mume wangu) pindi tunazungumza jambo fulani mfano kwenye tunanunua kitu.

6. Anapenda kuzira ovyo ovyo.

7. Anapenda kufanya vitu nusu nusu mfano akisema vitu vya ndani(mahitaji ya chakula) vimeisha na ukamwambia orodhesha hivyo vitu, utaona anasema "basi" ukimlazimisha anakutajia vichache halafu ukimpa hela, anaanza kusema tena na kitu fulani hamna, wakati unamuuliza ataje vyote alikuwa hataki.

8. Anapenda kupekua simu yangu ingawa nimeweka nywila anayoifahamu ila ukitaka kupekua simu yake, anakuambia "unanichunguza?" kwani huniamini? hapo na mimi namwambia kama hupendi kitu fulani basi na wewe usipende kumtendea mtu kitu hicho.

Yote tisa kumi upande wa uvumilivu ana grade A.
 
Nimesoma weeee....! Sijaona mtu anayekabiliwa na mapungufu ninayokabiliana!!

Nimeoa msichana mzuri, tulikuwa tunafanana tabia kama kupenda kusikiliza aina fulani ya music pamoja. Kutoka outing, kupiga wine zetu wenyewe daaah!! Tukisafiri itaandaliwa collection ya music na humo garini ni raha tupu.

Sijui kakutana na mitume gani pumbafu!! Wamemfanya amebadilika totally, amekuwa mwoga wa maisha, anaogopa kufa kama yeye ndo atakufa pekee.

Nyumbani!! Hakuna kusikiliza music ni dhambi, no wine no anything!! Nyumba ipo kimyaaa....!!

Hakuna utani hakuna stories muda wote ni kuomba na kulia mpaka namshangaa kilichomkuta!!

Hakuna kujipodoa wala kusukia nywele bandia, dhambi!! Kuna manguo yao kama sketi za charanga yaan!! Kawa kama bibi fulani hivi!

Muda wote ni serious! Mkali kwa watoto mkali kwangu japo nilishamuwasha kwangu mie haleti ujinga wake.

Imebidi niwashike watoto (nipo nao close) maana niliona wanakuwa victims kwa hii tabia iliyokuja. Naye nimemuacha ajiendeshe mwenyewe kwanza akirudi kawaida tutaelewana.

Maisha nimeamua kuyafanya kama naishi alone kwanza ili mambo yaende ila ni kero kubwa saaana!!

Kama ni muumini wa hawa matapeli wanaojiita mitume pole sana huyo kumbadili sio rahisi labda uamue kuwa mbabe flani humo ndani kusikalike kama ataenda kwa hao matapeli la sivyo kuna jingine
 
Back
Top Bottom