Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

1. Mbishi, anajibizana bila kuogopa

2. Hapendi kufokewa ila yeye analazimisha kufokewa kutokana na ubishi wake.

3. Anapenda kulia kuonesha kuwa kaonewa huku ndio yeye anasababisha

4. Upangilio wa nyumba na usafi kwa ujumla, anaweza kuacha kitu hakiko kwenye mahala pake kwa muda siku kadhaa, hadi umwambie ndio anakiweka mahali pake.

5. Nikiwa naye public anapenda kujionesha kuwa ana mume kwa kuniita ita(mume wangu) pindi tunazungumza jambo fulani mfano kwenye tunanunua kitu.

6. Anapenda kuzira ovyo ovyo.

7. Anapenda kufanya vitu nusu nusu mfano akisema vitu vya ndani(mahitaji ya chakula) vimeisha na ukamwambia orodhesha hivyo vitu, utaona anasema "basi" ukimlazimisha anakutajia vichache halafu ukimpa hela, anaanza kusema tena na kitu fulani hamna, wakati unamuuliza ataje vyote alikuwa hataki.

8. Anapenda kupekua simu yangu ingawa nimeweka nywila anayoifahamu ila ukitaka kupekua simu yake, anakuambia "unanichunguza?" kwani huniamini? hapo na mimi namwambia kama hupendi kitu fulani basi na wewe usipende kumtendea mtu kitu hicho.

Yote tisa kumi upande wa uvumilivu ana grade A.
🤣Na.5 hiyo Mimi kabisaa 🙌..aisee napenda kuonyesha umiliki mpk sio poa...na.2 pia....
Na.4,7...pole sn
 
Hahah mkuu tunasafiri boti moja!

Mimi sasa nimepanga niende kwa fundi anitengenezee draw ndogo yenye lock kwa ajili ya kuweka vitu vyangu vidogo vidogo,jumapili iliyopita nilikuwa home sasa kuna wakati nikahitaji kutumia kalamu nikatafuta zinakokaa nikakosa kuna sehemu kabatini huwa naweka pen ya dharura kwenda kuangalia haipo mara anaenda kuileta kutoka juu ya fridge jikoni.

Na sijui alijuaje kama pana kalamu maana niliificha,socks kupata pair inayofanana ndiyo shughuli zaidi naweza kukaa mwezi sijavaa socks zinazofanana rangi utakuta rangi moja ipo kabatini moja ipo kwenye kamba nje nyengine zimechanganyika kwenye nguo za watoto,ni changamoto sana.
Aiseee 🙌
 
Nashuk

Nashukuru kunipa moyo kaka,
Naamini ananipenda, ila kwangu ndio naona kero, akiwa mbali anaweza kuamka alfajiri anajiandaa basi urapigiwa simu, sasa wengine usimgizi mi starehe yetu kiukweli, nilikuwa natabia ya kuweka simu silent nikiwa nalala haswa mchana, ila ye akiwa mbali imebidi niache tu, maana alfajiri usipopokea simu itaonekana unapata morning glory sehemu 🤣😂
Huyo Mimi kabisa🙈🤭
Kwenye suala la cm
🙌
 
Wakuuu habari za usiku.

Moja kwa Moja twende kwenye maada. Mimi kwa upande wangu mapungu yafuatayo kutoka kwa mama watoto wangu nimekubali KUISHI NAYO.

1. Kuto pokea simu.
Mke wa Mimi hapokei simu hata aione inaita hatashughulika NAYO Hadi amalize shughuli zake. Ukimpigia simu asipo pokea usijisumbue kutuma sms, ukituma Kuna siku utaisoma mwenyewe.

2. Dawa ya mswaki.
Kwenye matumizi ya hii KITU yeye huminya popote pale.

3. Hajichanganya na WATU.
Yeye ni kazini, nyumbani na kanisani. Haendi tofauti na maeneo hayo labda kwenye mambo ya jamii.

4. Ukimkosea hakuulizi na haoneshi kama amechukia ila utaulizwa siku nyingine na atawasilisha kwa njia ya utani.

5. Akikukosea ukiuliza atakuambia nisamehe baba......... hapo hata uongee vipi hatakujibu.

Hapendi kabisaa kijichanganya na WATU hasa ukitaka umuudhi fika nyumbani anza kumwongelea mtu hapendi kabisaa na anachukia kwa dhati.

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo nimeamua KUISHI NAYO na nimefamikiwa KUISHI NAYO kwa muda wa miaka 19 ya ndoa yetu.
Mengi sana sana. Ila kama mimi ananivumilia. Ila nikijuwa kachepuka na Nina uhakika. HILO HALISAMEHEKI...
 
Back
Top Bottom