1. Mbishi, anajibizana bila kuogopa
2. Hapendi kufokewa ila yeye analazimisha kufokewa kutokana na ubishi wake.
3. Anapenda kulia kuonesha kuwa kaonewa huku ndio yeye anasababisha
4. Upangilio wa nyumba na usafi kwa ujumla, anaweza kuacha kitu hakiko kwenye mahala pake kwa muda siku kadhaa, hadi umwambie ndio anakiweka mahali pake.
5. Nikiwa naye public anapenda kujionesha kuwa ana mume kwa kuniita ita(mume wangu) pindi tunazungumza jambo fulani mfano kwenye tunanunua kitu.
6. Anapenda kuzira ovyo ovyo.
7. Anapenda kufanya vitu nusu nusu mfano akisema vitu vya ndani(mahitaji ya chakula) vimeisha na ukamwambia orodhesha hivyo vitu, utaona anasema "basi" ukimlazimisha anakutajia vichache halafu ukimpa hela, anaanza kusema tena na kitu fulani hamna, wakati unamuuliza ataje vyote alikuwa hataki.
8. Anapenda kupekua simu yangu ingawa nimeweka nywila anayoifahamu ila ukitaka kupekua simu yake, anakuambia "unanichunguza?" kwani huniamini? hapo na mimi namwambia kama hupendi kitu fulani basi na wewe usipende kumtendea mtu kitu hicho.
Yote tisa kumi upande wa uvumilivu ana grade A.