Ni matarajio ya pamoja ya dunia ya kusini kuona AU inakuwa mwanachama rasmi wa G20

Ni matarajio ya pamoja ya dunia ya kusini kuona AU inakuwa mwanachama rasmi wa G20

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG41N1342324354.jpg


Mkutano wa 19 wa Viongozi wa kundi la nchi 20 (G20) umefanyika nchini Brazil, ambapo Umoja wa Afrika umeshiriki kwa mara ya kwanza kama mwanachama rasmi, na kuwa shirika la pili la kikanda baada ya Umoja wa Ulaya. Katika miaka ya hivi karibuni, nguvu ya dunia ya kusini inayowakilishwa na nchi zinazoendelea na nchi zinazoibukia kiuchumi imeongezeka kwa pamoja na kuwa mwelekeo usioweza kuzuiliwa.

Kama bara lenye idadi kubwa zaidi ya nchi zinazoendelea, Afrika ni sehemu muhimu ya dunia ya tatu. Uanachama rasmi wa Umoja wa Afrika katika G20 unaonyesha ukuaji wa nguvu za Afrika katika pande zote na unabeba matarajio ya pamoja ya China na nchi nyingine za dunia ya tatu.

Kutokana na juhudi zake na washirika wa dunia ya kusini, Afrika leo limekuwa bara lenye uhai na uchangamfu.

Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Fedha la Kimataifa, ukuaji wa uchumi katika Afrika Kusini mwa Sahara unatarajiwa kuwa 3.6% mwaka 2024, na kuongezeka hadi 4.2% mwaka 2025. Katika masuala ya kimataifa, Afrika sio tena "nchi nyingi zilizo kimya" bali ni nguvu mpya ya mwamko.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, misimamo ya nchi za Afrika imevutia ufuatiliaji wa pande zote kuhusu masuala mbalimbali kama vile mzozo wa Gaza, mgogoro kati ya Ukraine na Russia, na mabadiliko ya hali ya hewa.

Lakini wakati huo huo, pia tunapaswa kuona kwamba Afrika bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika kufikia maendeleo.

Kwa mfano, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, asilimia 83.2 ya watu maskini duniani wanaishi Afrika Kusini mwa Sahara na Asia Kusini, na kati ya nchi tano zenye idadi kubwa ya watu maskini, tatu ni nchi za Afrika.

Mfano mwingine ni kwamba nchi za Afrika zinatoa asilimia 4 tu ya uzalishaji wa gesi chafu duniani, lakini athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni kubwa zaidi kuliko zile za nchi zilizoendelea. Katika kukabiliana na changamoto hizi, Umoja wa Afrika utatumia jukwaa la G20 kupaza "sauti za Afrika" na kujitahidi kupata haki zaidi za maendeleo kwa bara la Afrika na nchi zinazoendelea.

Kama moja ya nchi za dunia ya kusini, China daima imekuwa "mtendaji" katika kuhimiza maendeleo ya kisasa ya Afrika na kuongeza sauti yake kimataifa. Sio tu ni nchi ya kwanza kueleza wazi kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20, lakini pia Kupitia majukwaa kama vile Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China na Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika, China imejitahidi kusaidia bidhaa za Afrika kufungua masoko ya China na kimataifa. Katika mkutano wa 19 wa viongozi wa G20, Rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua nane za China kusaidia maendeleo ya kimataifa, karibu zote zitahudumia moja kwa moja maslahi ya maendeleo ya Afrika.

Ni dhahiri kwamba tofauti na baadhi ya nchi za magharibi ambazo zimezoea kujihusisha na siasa za kijiografia barani Afrika na kujaribu kushinda dunia ya tatu, China inatumai kwa dhati kuwa Afrika na washirika wengine wa dunia ya tatu watapata maendeleo na ustawi, na hii imeonyesha uwajibikaji wa kimataifa inaobeba China katika kutetea ushirikiano wa kusini na kusini.
 
View attachment 3155773

Mkutano wa 19 wa Viongozi wa kundi la nchi 20 (G20) umefanyika nchini Brazil, ambapo Umoja wa Afrika umeshiriki kwa mara ya kwanza kama mwanachama rasmi, na kuwa shirika la pili la kikanda baada ya Umoja wa Ulaya. Katika miaka ya hivi karibuni, nguvu ya dunia ya kusini inayowakilishwa na nchi zinazoendelea na nchi zinazoibukia kiuchumi imeongezeka kwa pamoja na kuwa mwelekeo usioweza kuzuiliwa. Kama bara lenye idadi kubwa zaidi ya nchi zinazoendelea, Afrika ni sehemu muhimu ya dunia ya tatu. Uanachama rasmi wa Umoja wa Afrika katika G20 unaonyesha ukuaji wa nguvu za Afrika katika pande zote na unabeba matarajio ya pamoja ya China na nchi nyingine za dunia ya tatu.



Kutokana na juhudi zake na washirika wa dunia ya kusini, Afrika leo limekuwa bara lenye uhai na uchangamfu. Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Fedha la Kimataifa, ukuaji wa uchumi katika Afrika Kusini mwa Sahara unatarajiwa kuwa 3.6% mwaka 2024, na kuongezeka hadi 4.2% mwaka 2025. Katika masuala ya kimataifa, Afrika sio tena "nchi nyingi zilizo kimya" bali ni nguvu mpya ya mwamko. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, misimamo ya nchi za Afrika imevutia ufuatiliaji wa pande zote kuhusu masuala mbalimbali kama vile mzozo wa Gaza, mgogoro kati ya Ukraine na Russia, na mabadiliko ya hali ya hewa.



Lakini wakati huo huo, pia tunapaswa kuona kwamba Afrika bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika kufikia maendeleo. Kwa mfano, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, asilimia 83.2 ya watu maskini duniani wanaishi Afrika Kusini mwa Sahara na Asia Kusini, na kati ya nchi tano zenye idadi kubwa ya watu maskini, tatu ni nchi za Afrika. Mfano mwingine ni kwamba nchi za Afrika zinatoa asilimia 4 tu ya uzalishaji wa gesi chafu duniani, lakini athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni kubwa zaidi kuliko zile za nchi zilizoendelea. Katika kukabiliana na changamoto hizi, Umoja wa Afrika utatumia jukwaa la G20 kupaza "sauti za Afrika" na kujitahidi kupata haki zaidi za maendeleo kwa bara la Afrika na nchi zinazoendelea.



Kama moja ya nchi za dunia ya kusini, China daima imekuwa "mtendaji" katika kuhimiza maendeleo ya kisasa ya Afrika na kuongeza sauti yake kimataifa. Sio tu ni nchi ya kwanza kueleza wazi kuunga mkono Umoja wa Afrika kujiunga na G20, lakini pia Kupitia majukwaa kama vile Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China na Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika, China imejitahidi kusaidia bidhaa za Afrika kufungua masoko ya China na kimataifa. Katika mkutano wa 19 wa viongozi wa G20, Rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua nane za China kusaidia maendeleo ya kimataifa, karibu zote zitahudumia moja kwa moja maslahi ya maendeleo ya Afrika. Ni dhahiri kwamba tofauti na baadhi ya nchi za magharibi ambazo zimezoea kujihusisha na siasa za kijiografia barani Afrika na kujaribu kushinda dunia ya tatu, China inatumai kwa dhati kuwa Afrika na washirika wengine wa dunia ya tatu watapata maendeleo na ustawi, na hii imeonyesha uwajibikaji wa kimataifa inaobeba China katika kutetea ushirikiano wa kusini na kusini.
Badala ya AU kuwa mwanachama ambayo itatuchelewesha kwanini mwanachama au mwenyekiti wa G20 asiwe Samia ili tufanikiwe haraka.
 
Back
Top Bottom