Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

monta

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2014
Posts
1,271
Reaction score
1,803
Wakuu habari za humu ndani.
Hivi ni maumivu gani makali zaidi ya mwili wa binadamu ushawahi ku experience au uliona mtu anapitia ukaona kabisa ni maumivu makali kwa binadamu.

Kwangu mimi ni maumivu ya tumbo,kuna siku niliwahi changanya pilipili kichaa na vitunguu swaumu nikabrend then nikanywa aisee maumivu niliyoyapata sitakuja kusahau.Niliona Israel huyu hapa kaja kunisalimia.Tumbo linauma asikuambie mtu.

Je ni ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?
 
Binafsi mimi mtu ambae nilimshuhudia akipitia maumivu.

Huyu dada alikuwa hospitali akiumwa saratani ya titi,

Titi lake lilikuwa limeoza kwa upande wa kwapa huku.
Huyu dada dawa ya kuzuia maumivu ilikuwa ikiisha nguvu alikuwa analia sana.
Alikuwa anaumia sana.
Inasikitisha sana.
 
Macho aisee .Mpaka ule msemo wa 'Afya yako ndio mtaji wako niliuona una maana'.Hela nilikuwa naziona kama mavi tu,mama bae alikuwa anakarangiza mapocho pocho lakini nilikuwa nahisi kama nakula tambala la deki tu.Macho yalikuwa yanauma mpaka yanakuwa yamoto.
Madaktari wapewe mishahara minono sana.Ntaandika barua ya pongezi kwa hospitali iliyonihudumia na nitawa CC mkurugenzi wa halmashauri mpaka mama Samia.
Oiii.
 
Binafsi mimi mtu ambae nilimshuhudia akipitia maumivu.

Huyu dada alikuwa hospitali akiumwa saratani ya titi,

Titi lake lilikuwa limeoza kwa upande wa kwapa huku.
Huyu dada dawa ya kuzuia maumivu ilikuwa ikiisha nguvu alikuwa analia sana.
Alikuwa anaumia sana.
Inasikitisha sana.
Acha nimeuguza mtu wa namna hii usiombee, anakwambia uchungu anaosikia ni kama wa kuzaa lakini Bora wa kuzaa mtu anategemea kupata mtoto unakuwa ni uchungu wa furaha lakini sio wa maumivu wa vidonda vya saratani hatari sana....
 
Back
Top Bottom