Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Wakuu habari za humu ndani.
Hivi ni maumivu gani makali zaidi ya mwili wa binadamu ushawahi ku experience au uliona mtu anapitia ukaona kabisa ni maumivu makali kwa binadamu.

Kwangu mimi ni maumivu ya tumbo,kuna siku niliwahi changanya pilipili kichaa na vitunguu swaumu nikabrend then nikanywa aisee maumivu niliyoyapata sitakuja kusahau.Niliona Israel huyu hapa kaja kunisalimia.Tumbo linauma asikuambie mtu.

Je ni ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?
Kuna Ile unalima afu mpini wa jembe ukugonge kwenye mguu mfupa wa mbele....sijui mnanielewa!
 
Kama umeenda Ocean Road Cancer Institute kumuangalia mgonjwa kuna wale waliofikia stage ya mwisho wanapigwa morphine tu kuwapunguzia maumivu, inasikitisha sana.
Hakika, hata huyu Dada alikuwa anatumia morphine ile ya syrup.

Upande mwingine kuna wale wana saratani ya koo.

Nadhani kwenye swala la maumivu wagonjwa wenye saratani wanaweza kuwa wanateseka zaidi pengine kuliko magonjwa mengine
 
Kuna siku nataka kusafiri kesho yake.. jicho from no where jamani likaanza kuuma..wee liliniumaaa jamanii liliumaaa nikaanza kulia ndo sasa nikahisi linaanguka..mpk saa 10 alfajiri nilishakata tamaa sisafiri tena moyo unaumaa..nilishaomba mpk basi...hatimae likapoa ila sijui ilikua ni nini mpk leo sijawahi pata ile hali

Tumbo nalo uwiiii kuna siku niliamka saa nne tumbo kama utani..likaanza jamani lile tumboo...sijui ni nini nilikua nasikia moyo unapigia hapo kwny mbavu....siharishi sitapiki...yani nahisi kufaa natambaa jasho linatoka...mwili wote...nikasema sasa nipige simu nitafia ndani...lakini kabla sijapiga simu nikasema ninywe maji..sijui ndo ilikua dawa ilee...likapungua kuuma mpk kupoa..

Maumivu ya kujifungua ni hatari sanaaa...sema huwa tunavikwa ujasiri na Mungu...

#Hakuna kitu kwny mwili wa binadamu ambacho hakiumi...##
Kuna siku na mie nliumwa na tumbo km hilo. Ilikuwa gesi sijui, maana nikitoka kula mihogo.
Ile siku niliona ndio naaga, unajiskia kwenda chooni ukifika hamna kitu, najiskia km kutapika lkn sitapiki, yaani huko chooni nilikuwa naenda kwa kutambaa. Nilimaliza dawa, matango, zaatari, maji ya uvuguvugu. Holaa
Mpk ikabidi nipelekwe hospital. Nilipata dawa maumivu yalipungua lkn like 3 days nilikuwa siwezi kutembea kimo changu lazima niiname, yaani nikisema nisimame wima tumbo chini ya kitovu km napitishwa visu
 
Mgonjwa cancer ya tezidume anaposhindwa kukojoa anapowekewa ule mpira wa mkojo. Aisee usiombe kuona, ule mrija(catheter) una urefu zaidi ya futi moja, unene kama kalamu ya speedo unapenyezwa kwenye tundu la mboo hadi ufike kwenye kibofu cha mkojo. Narudia kusema usiombe kushuhudia ama yakukute.
Nilitaka niandike yangu,nikaona hii nikasoma, nimeona nitulie kwanza mpaka mwili umesisimka.
 
Wakuu habari za humu ndani.
Hivi ni maumivu gani makali zaidi ya mwili wa binadamu ushawahi ku experience au uliona mtu anapitia ukaona kabisa ni maumivu makali kwa binadamu.

Kwangu mimi ni maumivu ya tumbo,kuna siku niliwahi changanya pilipili kichaa na vitunguu swaumu nikabrend then nikanywa aisee maumivu niliyoyapata sitakuja kusahau.Niliona Israel huyu hapa kaja kunisalimia.Tumbo linauma asikuambie mtu.

Je ni ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?
Kubinywa ngozi ya pumbu
 
Back
Top Bottom