Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Kuna siku nataka kusafiri kesho yake.. jicho from no where jamani likaanza kuuma..wee liliniumaaa jamanii liliumaaa nikaanza kulia ndo sasa nikahisi linaanguka..mpk saa 10 alfajiri nilishakata tamaa sisafiri tena moyo unaumaa..nilishaomba mpk basi...hatimae likapoa ila sijui ilikua ni nini mpk leo sijawahi pata ile hali

Tumbo nalo uwiiii kuna siku niliamka saa nne tumbo kama utani..likaanza jamani lile tumboo...sijui ni nini nilikua nasikia moyo unapigia hapo kwny mbavu....siharishi sitapiki...yani nahisi kufaa natambaa jasho linatoka...mwili wote...nikasema sasa nipige simu nitafia ndani...lakini kabla sijapiga simu nikasema ninywe maji..sijui ndo ilikua dawa ilee...likapungua kuuma mpk kupoa..

Maumivu ya kujifungua ni hatari sanaaa...sema huwa tunavikwa ujasiri na Mungu...

#Hakuna kitu kwny mwili wa binadamu ambacho hakiumi...##
Wa kwetu hakuna kitu kinauma ila mbupu ziweke mbali na watu wa ovyo.
 
Poleee sana.Mimi yalikuwa yote mawili sijui ningekuwa pekeyangu tu ingekuwaje .Ilifikia hatua nikawa nashikwa kupelekwa njee.Macho muhimu sana aisee.
Asante mkuu..pole na wewe..
Macho ni kiungo muhimu sana...
 
Fanya yote lakini kamwe usikalie pu-mbu au usilibane Kwa namna yoyote Ile!! Maumivu yake hayasimuliki na hayana mfano.

Nimemaliza kama hujawahi jaribu tu hata kuliminya uone
Wakuu habari za humu ndani.
Hivi ni maumivu gani makali zaidi ya mwili wa binadamu ushawahi ku experience au uliona mtu anapitia ukaona kabisa ni maumivu makali kwa binadamu.

Kwangu mimi ni maumivu ya tumbo,kuna siku niliwahi changanya pilipili kichaa na vitunguu swaumu nikabrend then nikanywa aisee maumivu niliyoyapata sitakuja kusahau.Niliona Israel huyu hapa kaja kunisalimia.Tumbo linauma asikuambie mtu.

Je ni ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?
 
Sio kambaku (mafuta makali) hyo inaumiza mpaka meno
Now nimelala naumwa kichwa upande wa kushoto around the left eye KMMK. kichwa kinagonga kama saa maumivu yake hayaelezeki aise. Nishazunguka hospital napewa tu dawa za kituliza maumivu dah.
 
Kinachouma zaidi ni kile ulichowahi kuumwa haswaa na kikakusumbia. Ndo Kila mmoja achokuja nacho hapa ninavyoona.

Ila kwa Mimi, ni ngiri....yaani hernia. Aisee nilijikuta natafuna mchanga bila kujua kama nafanya hivyo Hadi pale inaponiacha ndo najua kuwa kumbe nilikuwa natafuna mchanga. Siku nyingine nilijikuta natolewa uvunguni mwa kitanda, hata sijui nilifikaje. Nashukuru Sasa nimeshafanyiwa upasuaji na sina tena ugonjwa huo.
 
Binafsi mimi mtu ambae nilimshuhudia akipitia maumivu.

Huyu dada alikuwa hospitali akiumwa saratani ya titi,

Titi lake lilikuwa limeoza kwa upande wa kwapa huku.
Huyu dada dawa ya kuzuia maumivu ilikuwa ikiisha nguvu alikuwa analia sana.
Alikuwa anaumia sana.
Inasikitisha sana.
My thoughts are with her
 
Nilimshuhudia mgonjwa wa sikio akipiga kelele hata pale mtu anapopita tu na kuburuza ndala au mlango unapofungwa kwa nguvu....sijui ndo unauma zaidi?!!
 
Kila sehemu ya mwili wa mwanadamu ni chungu Sana inapouma.

Ila Mimi niliwahi kuumwa jicho wakati Fulani aisee maumivu yake usipime.
Ule usiku ulikuwa mrefu Sana kwangu.
 
Uchungu wa kuzaa aisee na ndio maana unaitwa uchungu duuu ni nusu ya kifo
 
Kuna mtu ame mention kuvunjika mfupa somewhere aisee hii issue dah hadi mwili umesisimka wazee... Nikiwaza sana huwa naona sisi binadamu ni nothing tu kwa jinsi tulivyo delicate hivi.
 
Uchungu wa kuzaa aisee na ndio maana unaitwa uchungu duuu ni nusu ya kifo
Na kwanini msiwe mnajifungua tu mtoto mmoja na kuapa kutokuzaa tena.
Nyie wenyewe mnasema kujifungua ni uchungu afu Unakuta mtu anazaa watoto Saba kuendelea😅
 
Utafiti rasmi unasema kuwa

"Childbith is the second most painful thing after being burned alive"

Kwa Kiswahili : UCHUNGU wa Mwanamke kuzaa ndio kitu cha pili kinachouma zaidi duniani, ya kwanza ni "Kuchomwa moto ukiwa hai"
 
Mgonjwa cancer ya tezidume anaposhindwa kukojoa anapowekewa ule mpira wa mkojo. Aisee usiombe kuona, ule mrija(catheter) una urefu zaidi ya futi moja, unene kama kalamu ya speedo unapenyezwa kwenye tundu la mboo hadi ufike kwenye kibofu cha mkojo. Narudia kusema usiombe kushuhudia ama yakukute.
Mkuu hujawahi fanyiwa opetation na kuwekewa catheter?
 
Back
Top Bottom