Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,219
- 4,608
Nakumbuka tulikuwa tunatoka kijijini Kibungo wilaya ya Kigamboni, tunaelekea Pemba Mnazi kuogelea.
Tulipokuwa tunaingia Pemba Mnazi, barabara imefunikwa na kivuli kikali cha miti mikubwa ya miembe.
Katikati ya kivuli ukatokea mwanga mkali sana kiasi cha kutufanya tusiweze kuona mbele.
Basi wale wamama niliokuwa nao wakaanza kukemea, mara mbele katikati ya barabara kakatokea kababu kamevaa nguo zote nyeupe, kana ndevu nyeupe, kamekaa chini barabarani.
Basi nilikuwa naendesha Mark ll Super Charger ya boss TAJIRI MKUU WA MATAJIRI, bwana ehh, kazee haka hapa, nikakwepe au nikagonge?
Ile nimekakwepa,, mara bonge la shimo hili hapa, ndio gari inaenda kuzama. Pongezi kwa wana maombi.
Tukarudisha gari nyuma, wananchi wanapiga miluzi kama yote, mna bahati sana nyie, huu ni muda wa majini kwenda kuswali, kweli MUNGU wenu ni mkubwa.